Nahitaji kuwekeza Tsh. Milioni 170

Hivi kwanini sasa hivi kila mtu anawaza kuwekeza UTT na BOT, ina maana mazingira ya kufanya biashara Tanzania yamekuwa magumu sana au purchasing power ya raia imepungua sana? Yaani hakuna anayewaza hata kuhusu fursa za export.
Mazingiravya biashara tz ni risk sana hiyo ndio options pekee kwa wengi wasio na ideas za biashara na misukosuko yake..
 
Kaka sio simple kihivyo Ku shinda bid ya bond au treasury bill sio rahisi-unaweza ukawa na fedha zako na usipate hiyo nafasi ya kuzinunua.
Zina ushindani sana,kila MTU anataka kula kwa mrija.
KwanzA huwezi kaa mwaka mzima ukakosa chance kwenye annual calenda nzima

Pili, ukishindwa kuingia direct kwenye BONDS za serikali BOT tumia utt AMIS ana mfuko wa Bonds Hela zake Huwa anawekeza kwenye Kununua Bonds za serikali.

Nadhani umenielewa.
 
Kama uko interested nipigie 0714 122 011
Nikupe mpango wa Jenga uza,
Utapiga mchele wa kutosha,
Biashara ambayo haina hasara kabisa,
Kama faida inaweza kuwa milioni 3 mpaka 4 kwa mwezi kuanzia tunaanza kujenga mpaka tunaiuza,
Piga simu
Jenga uza sio rahisi kiivo boss huwezi pata mteja kirahisi kwa faida nzuri maana kila mwezi upate mteja wa kununua nyumba si rahisi abadan.
 
mjinga mwenyewe,hicho ulichoandika unafikiri nani asiye kijua, nafikiri hukuipata point yangu vizuri tangu mwanzo umedandia tuu mada, mimi sijapinga mtu ku invest niliuliza miaka hii ya karibuni watu wengi wanakimbizia mitaji yao kwenye mutual funds na bot ni kwamba mazingira ya kufanya biashara tanzania yamekuwa magumu au watu ni wavivu wa kutafuta fursa mpya.?
 
Kunguni wewe ulisoma comprehension kweli wewe.
 
Usijaribu kufanya biashara yoyote huku ukiwa huna uzoefu wowote ule. Bora ukafuata tu ushauri wa wadau hapo juu.

Kaweke hiyo hela kwenye hiyo biashara ya hati fungani, ukishindwa kabisa basi tafuta eneo lenye wasafiri/mzunguko mkubwa wa watu; jenga lodge yako standard! Halafu weka cctv cameras, weka usimamizi makini! Halafu uje ulete mrejesho.

Ukiingia tu kwenye biashara! Sijui ya madini, mazao, kilimo cha matikiti, nk. Hiyo hela yote itapukutika.
 
Kwamba rejesho dogo au kubwa sana?
Kariakoo kuna watu hawana mitaji(wanatafuta wateja wanachukua mzigo mali kauli wanamake at least 150 kwa siku - though kuna siku wanakosa lakini leo ukipata 150k, unakaa siku 4 pakavu, unapata 2m siku 1, unakaa wiki pakavu, anothe day unamake 700k ukija wastani wa mwezi unakuta una at last 150 daily) na wanamake zaidi ya 3m kwa mwezi wamejenga nyumba hawafanani nazo ukiwaona utajua wameachiwa kulinda, sasa huyu ana m170 anataka 2M huoni ni hajawa well informed, yaani huyu biashara akianza si ajabu akaangukia pua.
 
Za jioni wadau,

Naomba mchango wa mawazo yenu, nikiwa na milioni 170 za kitanzania naweza wekeza wapi pesa hii nikapata rejesho lenye tija?

Kwangu mimi rejesho lenye tija ni angalau milioni 2 kwa mwezi.

Natanguliza shukrani.
Jiunge na Niffer atakusaidia
 
Kuna mtu anapigwa hapa. Kuwa makini kaka mwenye 170m
 
Wewe huna akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…