Ngoja nishibe kwanza , ntachangie baadae.
Nishashiba sasa nimerudi.
Microfinance bhana Zina changamoto nyingi kwa wakopaji. Wakopeshaji wanazo lakini sio sanaa kama wakopeshawaji.
Faida zipo kwa wote wawili yapo mmoja anafaidika zaidi kuliko mwengine.
Mmm nachangia kwenye hasara tu za Microfinance.
1. Kumfilisi mkopaji.
Mikopo hasa hii ya kausha damu humfilisi mkopaji kwa Ile riba. Riba inakuwa kubwa kuliko kiasi ulichokopa , unaweza kukuta unatoa faida sawa na Kiasi ulichopewa.
Mfano: unaweza kukopeshwa elfu 50, katika 50 hiyo hiyo wakakukata 15 ya fomu na vitu vingine, kwahy hapo wanakupa 35 yapo wao wanakupa 50 lakini kimahesabu uliwapa 15 Yako kwahy inakuwa wamekupa 35, kwahy badala ya kupanda juu unashuka kwakua faida Yako wanaibeba wao.
Marejesho Kila siku 2000 kwa siku 30 ni elfu 60, kwahy umepewa 35 unarudisha 60 , riba ni kubwa.
2. Inaharibu mahusiano.
Unakuta mke kakopa mume hajui, kashindwa Kulipa wamekuja kubeba vitu ugomvi unaibuka na kuvunja mahusiano.
3. Maisha kuwa magumu.
Mtu kakopa aongezee mtaji lakini riba kubwa marejesho yamemshinda wanakuja kusomba vitu , unaanza tena upya , mtaji huna na vitu huna maisha yanazidi kuwa magumu.
4. Watu kuhama miji.
Mtu akishindwa kulipa anaukimbia mji wake, anaona Bora aondoke akakae hata kwa shangazi ili tu adichukuliwe sheria kwa kushindwa kulipa mkopo wake.
5. Kuongezeka kwa watoto wa mitaani.
Mahusiano yakishaharibika, watu wakianza upya, miji ikihamwa na watu kinachofata watoto watazagaa kwa kukosa wa kuwalea au mahitaji ya shuleni , hivyo watoto wa mitaani wataongezeka.
6. Kuporomoka kwa maadili.
Watoto wa mitaani wakishajazana basi na maadili yanaporomoka kwa kuwa watoto hujilea wenyewe Hawana waangalizi wa kuwaelekeza mazuri na mabaya.