Nahitaji mkopo wa laki 1

Nahitaji mkopo wa laki 1

kokushobya

Member
Joined
Dec 13, 2015
Posts
19
Reaction score
10
Habari zenu wana JF, sorry guy mm nilikuwa nahitaji mtu au sehemu ambayo naweza kupata mkopo wa 100,000 nahitaji kujiajiri mwenyewe nifanye biashara,naomba msaada wenu
 
Piga namba hii fasterrr utapata mkopo - 0712276855
 
Habari zenu wana jf,sorry guy mm nilikuwa nahitaji mtu au sehemu ambayo naweza kupata mkopo wa 100,000 nahitaji kujiajiri mwenyewe nifanye biashara,naomba msaada wenu

Seriously? unataka kujiajiri na kufanya biashara kwa kuanzia na laki moja? au unamtaji wako ila ni kasoro hiyo laki moja unayotaka upewe mkopo?
 
Habari zenu wana jf,sorry guy mm nilikuwa nahitaji mtu au sehemu ambayo naweza kupata mkopo wa 100,000 nahitaji kujiajiri mwenyewe nifanye biashara,naomba msaada wenu
Mikopo midogo hiyo unatakiwa usisumbue mtu kopa tigo pesa Airtel Money nk unabofya tu kwenye simu yako pesa zinaingia za mkopo. Hukopesheki hata kampuni za simu?
 
Mikopo midogo hiyo unatakiwa usisumbue mtu kopa tigo pesa Airtel Money nk unabofya tu kwenye simu yako pesa zinaingia za mkopo. Hukopesheki hata kampuni za simu?
aise,umenichekesha sana ulivyouliza hapo mwisho...kwamba hata mitandao ya simu inshindwa kumkopesha?
 
Kama upo mbeya mjin, weka namba yako hapa ntakucheki soon
 
mitandao ipi inakopesha 100k kwa mara ya kwanza??...acheni hizo bhana
Unatakiwa kuanza kidogo kidogo unakopa unarudisha hadi ufikie juu wakipima uaminifu wako.Watu wanakopa hadi laki 5 kirahisi tu.Enzi za kuzurura mji mzima unamtafuta mtu wa kukukopesha elfu 20 au hata laki umepitwa na wakati
 
Mtaji ni wazo lako kichwani, ondoa mawazo ya laki moja ukopeshwe kwanza ili ufanye ulichokibuni. Tunategemea una umri chini ya 25, kama hivyo ndivyo kuna kazi kibao za kufanya kuipata hiyo laki moja kwa wiki. Kama una zaidi ya miaka 25 basi wewe ni tatizo tayari maana unachokiomba hakiendani na umri wako.

1. Unaweza kuuza maji ya madumu -
2. Unaweza kuuza mayai ya kuchemsha unatembeza
3. Unaweza kwenda kwenye viwanda vidogo vidogo vyya kufyatulia matofali - kazi kibao kuyapanga, kupakia n.k
4. Unaweza kwenda kwenye vijiwe vya kuoshea magari - kazi mbwerere pale nguvu zako tu
5. Unaweza kutafuta kijiwe cha chipsi, ukajishikiza ukaanza hata kumenya viazi na kusaidi kugawa sahani kwa wateja nk

Kazi ni nyingi mno za kupata hiyo laki moja ya kuanzishia mradi wako - jiongeze kijana fainali huwa uzeeni mdogo wangu.
 
Back
Top Bottom