Kwa mtu anayeeelewa mikataba kisheria, riba hii iko juu mno kiasi kwamba ni risky mtu kukukopesha kiasi hicho kwa riba hiyo halafu mkatengeneza mkataba kisheria (una bond na hiyo inaashiria kuwa unataka mkopeshane kisheria).
Tuseme ukishindwa kumrudishia halafu ukaja ukamruka kuwa wakati mnafanya makubaliano akili yako haikuwa sawa sawa, yaani ulikuwa insane, kuna uwezekano ukaja kumshinda kesi. Kumbuka insanity huwa ni mchawi wa mikataba. Riba kubwa kiasi hicho inaweza ikaingiwa kwenye makubaliano na watu ambao mmojawapo ni minor au ni insane, kitu ambacho huwa kina-diqualify mkataba outright!