NyegereBOY
JF-Expert Member
- Mar 24, 2021
- 302
- 520
- Thread starter
-
- #41
nimekuelewa chief lakini kuna kitu kimoja tunatakiwa kuelewa wote kwa pamoja hata mimi sikuwahi kuelewa mpaka nilipopata maarifa ambayo yalitokana na kufanya research mbalimbali na ku take risk acha nielezee kwa kifupi hotspot ilivyo najua kwa wengi ni kitu kigumu kwakuwa ni kigeni hasa nchini ila kwa kenya na uganda au bara la asia ndiko zimeenea zaidiBiashara yako haina RISKS?
Hujajadili potential risks kwenye biashara hii.
Ushauri: Wenda una wazo zuri lakini unashindwa kuliwasilisha vyema, au hujajua unahitaji nini. Mwekezaji/Investor sio Mhisani/Donor/Funder. Ukimweleza mwekezaji makini, aweke 50M, kwa ROI ya miezi sita, ataona wazi unataka kumwibia. Mwekezaji analenga kupata usalama hasa wa pesa yake kabla ya faida. Yaani unapochukua pesa ya mwekezaji cha kwanza ni usalama na uhakika wa pesa yake, afu faida. Kwa lugha nyepesi, akikosa hiyo faida, pesa yake itakuwepo. Au ndio mtaanza kudaiana na kupeana majina yasiofaa.
Hujaeleza risks ya biashara yako, hujaeleza ni vipi pesa ya mwekezaji takuwa salama katika mikono yako. Umevutia tuu faida.
Do your homework, wawekezaji makini hawataki kusikia kuhusu faida, wanataka kusikia kuhusu usalama wa fedha zao zikiwa mikononi mwako "How safe is the money.
Hii ndivyo ilivyo na huua ndoto nyingi za wafanyabiashara wengi kwakuwa hatuna platform maalum au funds za startup inatuwia ugumu na ndio mana tunaleta kwa wadau mbali mbali tunaweza tusipate hela ila tukapata njia mimi kufanikisha hii biashara pia kunamsaada pia nilipata kupitia jukwaa hiliHakuna benki inatoa mtaji wa mwanzo "Initial capital" benki inatoa endelezo la mtaji "Working Capital".
Akienda benki, watamwambia biashara iwe na miaka mitatu, iwe na leseni, awe na akaunti ya biashara, awe na mizania ya hesabu za biashara "Financial statements".
Mwisho watamwambia awe na dhamana sizizo hamishika.
Hotspot business ni biashara inayoingiza faida ya haraka nadhani kwasasa kuliko biashara nyingi hivo lengo kuu ni lilikuwa kukaribisha muwekezaji au yeyote mwenye mtaji kuweza kuiona fursa na kunufaika ila ukiwa na hata 2,500,000 unaweza kuifanya as individual kama mimi ninavyofanya sasa na sio kwamba sinufaiki nina nufaika nayoJustification ya kuanzisha at least 20 sites ni nini?
Safi sana.mkuu naomba nikukanushe kidogo hii biashara mimi naifanya kwa muda wa miaka 2 sasa kila nilichoandika sio fikra ni uhalisia na nakuruhusu kuja kuuushuhudia ngoja nikujibu swali moja baada ya lingine
ukiifahamu vizuri hotspot business haisumbui hata kidogo tofauti na wengi wanavyodhani
1. kwanza kabisa aina ya hotspot business nayo ifanya tofauti unayoijua wewe ya kuunga mtu kwa kutumia password hiyo kitu ni ya zamani sanaaa kwa sasa kuna mifumo inafahamika kama hotspot billing system ukipata nafasi google mkuu upate elimu zaidi
2 ushindani biashara hii kwa Tanzania badooo sanaaaa wanaofanya ni wachache mno na wengi wao wanaofanya niwale wenye CPE yake mfano kanunua ya airtel ndio anafanya ila mimi nafanya ina a large scale naweza ku deploy system hadi ya urefu wa kilometer moja moja na hii inanifanya niwe tofauti na zingine
3.TTCL kukata line kwanza kabisa bahati nzuri mimi main hustle yangu nauza unlimited internet kama partner wa mtandao moja wapo wa simu hapa nchini hivo internet providers ni wengi sanaaa na kuna kitu nimeandika hapo juu kinaitwa GATEWAY ukipata nafasi kaisome ujue inafanya nini
4. KODI ya eneo nafikiri picha ulionayo ya hotspot inavofanyika na uhalisia hauko hivo kabisa mfano mimi nimefunga hotspot maeneo mengi na hiyo code haipo mana kinachofungwa ni acccess point sasa nenda kaangalie access point ilivyo kisha niambie kodi stahiki ya kulipia it is imposible mkuu na sitoi kichwani ninafanya tayari hii biashara
5. kulipa wa simamizi hii sasa ukitaka kuielewa zaidi nakukaribisha site kwakuwa hapa ningumu kuweka kila kitu ila kifupi kuna agent ambao mimi nawauzia kila mmoja 10 vouchers kwa 5,000 then wao wanauza kwa 1,000 kisha wanapata 10,000 yao hivo faida 5000 ambayo wanajilipia umeme wenyewe easy sana mkuuu tofauti unavyofikilia
6. Uharibufu upotevu maintainance hii nimejibu na nakujibu tena kuwa hii biashara tofuti na unachofikiria nimefanya biashara hii na sitezote maintainace nafanya mwenyewe why ? kwakuwa na mudu hivo vyote mwenyewe bila ya kuongeza mtu nimekuweka na database inayoniwezesha kufuatilia wateja wangu
7. Revenue proof mkuu utaweka kila mahali kama nyanya si ndio mana muwekezaji anaruhusiwa kutembelea site na kujionea tatizo ni moja umekuja kwa negative energy tutulie tujifunze kwa pamoja
hili ni tatizo la confidance ikichanganyikana na ujinga Ungekuwa unafanya hii biashara ungeielewa zaidi ila kifupi kama ni muwekezaji nakukaribisha site
Mgerasi yule mshangazi leo ndo amekuachiaHauna pesa bwashee acha kusumbua uma
Unasema unanunua internet kwa malipo ya 200,000/= kwa mwezi. Hiki kiasi hakitegemei usage (i.e., ni gharama ya unlimited plan)?Hotspot business ni biashara inayoingiza faida ya haraka nadhani kwasasa kuliko biashara nyingi hivo lengo kuu ni lilikuwa kukaribisha muwekezaji au yeyote mwenye mtaji kuweza kuiona fursa na kunufaika ila ukiwa na hata 2,500,000 unaweza kuifanya as individual kama mimi ninavyofanya sasa na sio kwamba sinufaiki nina nufaika nayo
nina ndoto kubwa ya kuikuza hii biashara na kuwa wakwanza sokoni au watu wa mwanzo kusambaza biashara hii lakini mimi binafsi siwezi kufika huko kama kilaa kitu nitafanya mwenyewe ilihali kuna wadau wenye mitaji na hawajui ni wapi pa kuwekeza kama muwekezaji anamtaji mdogo huwa nampa fursa ya kufanya yeye mwenyewe kama nilivofanya kwa wengi
Andika andiko uwapelekee benkiNatumaini ni wazima wa Afya na heri ya mapumziko ya mwisho wa mwaka
Najua mwaka huu ulikuwa na changamoto nyingi na baadhi yetu tulikuwa na malengo mengi naimani kwa uwezo wake M/Mungu mwaka ujao tutakamilisha au kuanzisha ndoto tulizoacha
Nisiwachoshe sana kwa salamu ni kama kichwa kinavyojieleza hapo ya kuwa nahitaji muwekezaji wa kuwekeza milioni 50 katika hotspot business, mtaji utarudi ndani ya miezi 6 na ataendelea kupata gawio la milioni 5 kila mwezi
Kwanini naandika hili ni kwakuwa naimani sisi katika kujaaliwa ridhki tumetofautiana naimani kuna mtu ana kiasi fulani cha fedha na hajua wapi pa kuwekeza au hana mtu sahihi wa kumshauri kuwekeza, lakini pia kuna akina sisi tuna mawazo mbali mbali ya kibiashara lakini hatuna mitaji ya kuwekeza
Hivo basi lengo la uzi huu ni kumfikia yule mwenye mtaji ila hajui wapi pa kuwekeza ili tuweze kushirikiana na kulisongesha gurudumu la mafanikio kwa pamoja.
Turudi kwenye mada Husika ni kuwa nahitaji muwekezaji wa kiasi kisichopungua 50 millioni kwaajili ya biashara ya HOTSPOT BUSINESS
Nini maana ya HOTSPOT ?
Hotspot Ni sehemu ambayo inakupa muunganisho wa internet kwa kutumia WI-FI bila kutumia nyaya
Nini maana ya WI-FI ?
Kwanza kabisa tufahamu kirefu cha neno WI-FI (Wireless Fidelity)
Wireless Fidelity ni teknolojia inayotumika kuunganisha vifaa kwenye mtandao wa internet bila nyaya
sasa kwakuwa tumeshafahamu maana ya hotspot na maana ya wi-fi sasa turudi kwenye mada ili twende sawa
Nini maana ya HOTSPOT BUSINESS ?
Hotspot Business ni biashara ya kuuza Huduma ya internet kwa njia ya WI-FI katika eneo fulani kwa malipo au makubaliano maalumu, sehemu hizo ni kama mtaani,sokoni,vyuoni na eneo lolote lenye mkusanyiko wa watu
kwa maelezo ya ziada biashara ya hotspot hufanyika katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu eidha ni wakaazi wa eneo husika au mahala pa biashara ambao watu hukutana na kushinda muda mrefu eneo hilo kwa siku zote mfano stand,sokoni,mtaani
unaweza pitia uzi wenye kichwa cha habari hichi kuongeza ujuzi zaidi Tengeneza hadi 50,000/= kwa siku kwa kufanya biashara ya kuuza internet kupitia WiFi kwenye maeneo yenye mkusanyiko
sasa basi kwakuwa tumeshafahamu nini kusudio la huu uzi sasa tuangalie huo mchananuo wa uwekezaji unao hitajika kiujumla mpaka ukafikia thamani hiyo tajwa hapo juu
ili kufanikisha biashara ya hotspot kuna vitendea kazi uhitajika kwaajili ya kukamilisha biashara hii ya Hotspot
1. Internet ( Hutolewa na kampuni za mawasiliano kama TTCL,HALOTEL,TIGO n.k )
2. Router ( Huuzwa madukani au hutolewa na kampuni za mawasilaino ukinunua huduma zao )
3. Gateway ( Huuzwa madukani )
4. Access Point ( Huuzwa madukani )
sasa basi ukiwa na vifaa tajwa hapo juu tayari unakuwa na vitendea kazi maalumu kwaajili ya biashara ya Hotspot sasa naomba nikupe hesabu kwanini inahitajika 50 milioni
Mimi ni miongoni mwa watanzania wachache tuliopata fursa ya kuutambua uwekezaji huu adimu hapa nchini na wenye faida ya uhakika na kwabahati nzuri tunafanya na kunufaika hadi sasa na lengo la kutafuta uwekezaji ni kuona namna gani tunaweza kufikia masoko zaidi ili kutengeneza faida zaidi
ili upate faida kubwa katika biashara ya hotspot yakupasa kufanya uwekezaji mkubwa
MFANO makadirio ya faida inayoweza kupatikana katika biashara ya hotspot kwa uwekezaji wa kiasi cha milioni 50 na hii sio makadirio ya kichwani ni kutokana na uzoefu na muundo wa biashara hii ambayo tayari nimeifanya kwa makadirio ya miaka miwili sasa
tumeona hapo juu mahitaji halisi ili kufanikisha biasharA hii ya hotspot ambayo ni
internet ,Router ,Gateway ,Access point sasa hii hotspot huwa tunafunga kwa site sasa ngoja tuone site moja inahitaji mtaji wa kiasi gani
MTAJI KWA SITE MOJA YA HOTSPOT
Vitendea kazi vinavyohitajika
internet nanunua kwa 200,000/= malipo ya kila mwezi
Router nanunua kwa 250,000/= malipo ya mara moja
Gateway nanunua kwa 150,000/= malipo ya maramoja
Access point nanunua 1 kwa 350,000/= hivo kwa site moja uhitajika 5 ambazo ni sawa na 1,750,000/=
Extra accessories (erthenet,RJs,climper,cable tie ) nanunua 150,000/=
kwa mchanganuo huu tunapata jumla ya Tsh 2,500,000/= za uwekezaji katika site moja
hivo basi tukirejea kwa dhumuni letu la kupata muwekezaji wa kiasi cha Tsh 50 milioni tunakusudia kupata mtaji wa kuweza kuanzisha sites 20
sasa hela inapatikana vipi kwa site moja ?
kwa namna mimi ninavofanya kwa site moja naweza kukusanya 40,000 kimo cha chini kwa siku 30,000
sasa kwakuwa tunahitaji muwekezaji wa kutupa mtaji wa 50,000,000 ambao ni sawa na site 20 tunaweka makadirio kila siku kwa site moja ikusanye kiasi cha 25,000 tu hii inamaanisha kwa site zote 20 tutakusanya 500,000 kwa siku
yaani kimahesabu 20 x 25,000 = 500,000 kwa siku
tukichukua makusanyo ya siku kwa mwezi ni sawa na
500,000 x 30 = 15,000,000/= Makusanyo kwa mwezi
tukitoa matumizi ya lazima ya kila mwezi kama nilivoainisha hapo juu ni malipo ya internet kwa mwezi
ambapo kwa site moja tumeona ni 200,000 kwa mwezi hivo kwa site 20 itakuwa
200,000 x 20 = 4,000,000 hii ndio gharama ya mwezi
kwakuwa tumeona kuwa kila mwezi tunahitajika matumizi ya internet basi tutachukua makusanyo ya jumla na kutoa matumizi ya lazima
15,000,000 makusanyo ya jumla mwezi mzima
4,000,000 malipo ya internet kwa mwezi mzima
15,000,000 - 4,000,000 = 11,000,000 kiasi kinachobaki
sasa kwanini tulisema kuwa muwekezaji wa kiasi cha Tsh 50,000,000 ataweza kurudisha mtaji wake kwa muda wa miezi sita na kuendelea kula faida kila mwezi isiopungua ya 5,000,000 ni kwa hesabu hii
kwakuwa tumeona kiasi ambacho kitaweza kubakia kwa mwezi ni 11,000,000 au 10,000,000 basi tutachukua hichi kiasi na kuzidisha mara 6 muda ambao tumeweka maximum muwekezaji kurudisha mtaji wake
kwaio
10,000,000 x 6 = 60,000,000/= au tunaweza weka makadirio ya 50,000,000/=
Hapo tutakuwa tumefanikisha kurudisha kiasi cha mtaji wa muwekezaji kilichobaki ni muendelezo wa safari ya kufurahia matunda ya uwekezaji wake ambao sisi tumeona iwe nusu ya faida itakayopatikana kwa kuthamini mchango wa muwekezaji kwa kuweka mtaji na sisi kuweka ujuzi wetu katika fursa hii
ambapo kama kwa mwezi makusanyo baada ya kutoa kila kitu kubakia 10,000,000 basi nusu itakuwa ya muwekezaji na nusu itskuewa ya kwetu sisi
JE NIKIWA KAMA MUWEKEZAJI NA UHAKIKA GANI WA KUREJESHA MTAJI WA PESA YANGU ?
Ukiwa na swali kama hili mimi nitakujibu hivi
inawezekana kurejesha hicho kiasi kwa muda kusidio kwakuwa hii ni biashara ya kisasa japo ngeni kwa macho ya wengi ila mimi nina uzoefu nayo kwa muda wamiaka miwili sasa na bado ninaifanya mpaka sasa hivo kumbukumbu za makusanyo yote katika site zangu yapo na tunamfumo wa kisasa kusimamia biashara hii mahali popote Tanzania hivo muwekezaji anauwezo wa kuona na kutambua kila kinachoendelea katika mfumo mahali popote alipo
lakini pia tunatoa fursa ya kutembelea mradi ulipo ambapo tunapatikana Dar es salaam na baadhi ya mikoa tumefunga hivo unaweza kujionea jinsi tunavyoendesha biashara hii na namna faida inavyoweza kuaptikana
Kwa wale wenye ndugu jamaa na marafiki ambao unaimani wanamitaji ila hawaoni pa kuwekeza tunawakaribisha muweze kuuliza maswali na tutajibu kila moja na kwa yule anaehitaji kuwekeza basi usisite kuwasiliana nasi kupitia 0710020066
200,000 ni kiasi kinachoweza kutosha kununua 100Mbps hadi 200Mbps inategemea kama utakuwa umechukua kwa wireless router itakuwa ni 100Mbps ila kama ni fiber unaweza kupewa 200MbpsUnasema unanunua internet kwa malipo ya 200,000/= kwa mwezi. Hiki kiasi hakitegemei usage (i.e., ni gharama ya unlimited plan)?
ingekuwa rahisi hivo mkuu naimani hata huu uzi tusingefanikiwa kuuandika ni kutokana na sheria ngumu tulizonao kwa wajasiriamali wadogoAndika andiko uwapelekee benki
Wakikupa hela unishtue
ni kweli unalosema hata ujuzi wa hii huduma nusu nilipata kupitia watu wa kenya aina ya Hotspot inayofanyika kesnya na hii nayo ifanya mimi ni tofauti kidogo mimi nafanya sana wireless ila wengine hutumia cable na hii ndio inanipa nafasi ya kuifanya coverage kubwa kwa aina hii nayo fanya imekuwa na nafasi katika nchi za wenzetu kwa muda mrefu sana mana Hotspot bussiness inanjia zaidi ya 20 ya kuifanya ni kuchagua kulingana na mazingira halisi kwa Tanzania ISPs KUJA Kufanya hotspot ni bado sana kwakuwa bado huduma ya FWA inawalipa zaidiHii biashara inaitwa Internet service provider ( ISP) Ni eidha uwe na kampuni la mawasiliano au mtu binafsi ulie na acces ya mtandao na unataka kusambazia watu
Ni sawa na na ile biashara ya cable upande wa TV.
Kwa bongo bdo kuna nafasi soko lipo ila kadli watu wanavyo nunua hzi router za mtandao biashar yako inakua inaenda chini pia TTCl wana hizi ethernet cable za internet wanafunga majumbani hii inafanya biashara yako kuwa limited japo bdo ipo valid kwa soko la Tz.
Kabla ya ujio wa starlink kenya vijana wenye wazo kama lako walikua wanfany biashar hii ya internet service provider kwa kuunganisha majumban hizi waya cable za ethernet na ku charge pesa kwa mwezi kama vile huduma ya cable kwenye Tv ilivyokua wakat huo ving'amuz vilipo kua vichache n havijasambaa nchini. Ujio wa starlink uliua au kudidimiza biashara y kwa sabab bei yake ilikua chini na speed yake ilikua ya kasi.
Wazo lako ni valid ila inabidi ue makini na big fish awa wenye makampun ya mitandao y simu voda, yas etc kwani wski copy unachofany bas uwekezaj unayumb.
Nazani fanya tafit zaid kwenye downfall ya awa ISP wa kenya kwani wao walikuw n nyaya na nguzo zao na miundombin walikuw nayo japo soko lao liliyumba.
All in all . Wazo lako bdo linawezekan cha msingi ni kupamban n risk
Watu 50 - 70 for how long? Haijalishi kama wanakesha online/streaming?kwa wastani package ya 100Mbps inauwezo wa kuhudumia watu 50 na zaidi mfano mimi kuna site naunga watu hadi 70 kwa 100Mbps na inafanya kazi bila shida
kwa maelezo inaweza kuonekana ndoto ila ninahakika kwakuwa hii sio wazo ni biashara ninayoifanya na niliowawezesha wengine kufanya pia mkuu ingekuwa nikitu cha kufikirika au ambacho hakijafanyika ningeweza kuafiki kile unachokizungumza ila kwakuwa nakifanya najua masoko yake changamoto na faida zako najiamini kwa kusema kuwa inawezekana uwekezaji wangu mimi nilirudisha kwa miezi 4 na hadi sasa naendelea kupata faidaMmmg seems to Good to be true. Ni kweli wateja wa Wifi. I wengi kiasi hicho uwe na uhakika wa kurejesha bdani ya Miezi sita?
Anza kutarget hostel z wanavyuo ata Kkoo ili kupunguza muda wa return on investmentni kweli unalosema hata ujuzi wa hii huduma nusu nilipata kupitia watu wa kenya aina ya Hotspot inayofanyika kesnya na hii nayo ifanya mimi ni tofauti kidogo mimi nafanya sana wireless ila wengine hutumia cable na hii ndio inanipa nafasi ya kuifanya coverage kubwa kwa aina hii nayo fanya imekuwa na nafasi katika nchi za wenzetu kwa muda mrefu sana mana Hotspot bussiness inanjia zaidi ya 20 ya kuifanya ni kuchagua kulingana na mazingira halisi kwa Tanzania ISPs KUJA Kufanya hotspot ni bado sana kwakuwa bado huduma ya FWA inawalipa zaidi
Toto tundu unaturingishia furaha yako ya krismas na demu wako mwajuma ndala ndefu?Kijana acha kwanza tufurahie X-Mas kwa amani wakati huu, mwaka umekwisha tukutane mwakani.