Nahitaji mwekezaji wa kuwekeza milioni 50 katika Hotspot Business, mtaji utarudi ndani ya miezi 6

Okay kama unauzoefu ni sahihi. Nikajua ni wazo ambalo ndio unaanza kutafutia wateja
 
Watu 50 - 70 for how long? Haijalishi kama wanakesha online/streaming?
kwakuwa mimi nawapa vocha ambayo inakuwa na duration ya muda wa masaa 24 hivo mteja anavyonunua akishajiunga itaanza ku count masaa yakifika 24 yatamtoa kwenye huduma rejea picha hapa chini nimekuwekea jinsi navyo weza kuona mteja amenunua vocha na kujiunga muda gani na itaisha mda gani

na ninawapa unlimited internet access kwaio wao wanaperuzi wawezavyo ila ukomo wa muda ni masaa 24
 

Attachments

  • Screenshot 2025-12-21 210846.png
    203.4 KB · Views: 37
Anza kutarget hostel z wanavyuo ata Kkoo ili kupunguza muda wa return on investment
mkuu sitafuti maeneo natafuta wawekezaji maeneo yapo mengi mnoooo na sio Dar es salaam ni Tanzania nzima kwaio tunawatafuta kisha wao waweze kuwekeza katika maeneo ambayo yanasubiria hiyo huduma
 
Hongera mkuu.
Inaonekana uko vizuri kwenye masuala ya tech,
Infact umenipiga gap hapo.

Hata hivyo hiyo siyo sababu yenye mashiko ya kuprove how inawezekana kupata ROI ya 6 months na 5M profit per month.

Mimi kama Investor ntahitaji proof, legal safeguards, audited financials na contingency plan.

Hiyo confidence yako + experience inatakiwa ilete advantage na siyo maelezo matupu.

Tatizo mkikutana na majibu ambayo hamkutarajia mnakimbilia kusema "Negative energy".
Weka hisia pembeni tujadili hoja kwa hoja.

Kama unabaki unashikilia assumptions zako bila proof kwa investor kama mimi hiyo ni high risk speculation, siyo investment yenye uhakika.
 
ANza kuweka 10M upewe equity ya 10% ya kila mtakachoingiza. Kisha utaendelea kuwekeza pesa iliobak mpka ifike io 50M
 
ni kitu kizuri na ndio maana tunasema kama ni invester unakaribishwa inafanyika survey tunakaa mezani yanafanyika makubaliano ya kimkataba na hata invester anaweza kujaribu kwa kuanza na kidogo kikimpa matokea anaweza kufanya zaidi lakini kila kitu hakiwezi kufanyika hapa thats why hii ni kama introduction lengo hasa ya hiyo hela ikatumike wapi na kivipi
 
ANza kuweka 10M upewe equity ya 10% ya kila mtakachoingiza. Kisha utaendelea kuwekeza pesa iliobak mpka ifike io 50M
Siwezi kulipa shillingi yoyote kwa projection tu au post kwenye forum.

ROI lazima ihalalishwe na data halisi na si maneno ya ushawishi.
 
ANza kuweka 10M upewe equity ya 10% ya kila mtakachoingiza. Kisha utaendelea kuwekeza pesa iliobak mpka ifike io 50M
Yes hii ni sawa kabisa kwa yule mwenye hofu unaruhusiwa kujaribu ili kuona namna mradi mzima unavyoweza kuendesha asanteh mkuu kwa kuirahisisha zaidi
 
Sasa tunaenda sawa.
Kama mwekezaji kila hela inapaswa kuangaliwa wapi inaenda na jinsi itakavyolindwa.
 
Siwezi kulipa shillingi yoyote kwa projection tu au post kwenye forum.

ROI lazima ihalalishwe na data halisi na si maneno ya ushawishi.
hivi vitu vipo lengo la kuandikwa uzi huu sio kukushawishi kwa maneno kukupa picha nini kinaenda kufanyika na kitafanyika vipi upo serius kwenye investment kuna meza ya mazungumzo kutembelea project kufanya analysis kisha muafaka unafikiwa mkuu hivo ndio biashara navo ona hufanyika
 
Sawa,
Nimehifadhi contacts.

Nitawatembelea muda wowote, lakini kwa lengo la kujifunza na kuona system,
Si kuwekeza bado.
 
Unasema unaingiza 1.5 m per month kama profit na upo kwenye game mwaka wa pili sasa si hiyo faida unayopata si upanue vijiwe uendelee kupiga pesa zako?
 
Unasema unaingiza 1.5 m per month kama profit na upo kwenye game mwaka wa pili sasa si hiyo faida unayopata si upanue vijiwe uendelee kupiga pesa zako?
unachokiwaza nisahihi kabisaa lakini kanuni ya maisha au mafanikio haiko hivo

kanuni halisi inasema hivi kama unataka kuanza haraka anzaa peke ako
kama unataka kufika mbali nenda na mwenzio

mimi nilianza mwenyewe nikaona fursa nikafanya inanipa faida lakini pia hiyo hiyo faida inanisaidia kuendesha maisha ya kila siku na kujikimu kwaio sio rahisi unavosema kwakuwa napata 1.5m basi nawekeza yote hapana

Na kwanini nitake kufanya kila kitu mwenyewe ilihali kuna watu wana hadi milioni 200 na hawajui pa kuwekeza anatamani apate wazo na hana na watu wote wakubwa waliofanikiwa hutumia hii kanuni
 

Mkuu kwanza nashukuru sababu umetaka kujifunza.
Pili hakuna Risks ya kufikirika. Kwenye hii biashara wewe ndiye mtaalam, na ndio Business Manager, wewe ni binadamu lolote linaweza kukupata na lika athiri biashara.

Hii ni biashara, inaweza zaliwa, ikakua na ikafa pia.

Ushauri: Hebu fanyia kazi ushauri ufuatao, kama utataka mwekezaji makini na kusiwepo uswahili.
Basi kubali kwamba wewe huna mtaji ila ndio mwenye wazo, kubali biashara hii ifanyike kupitia kampuni iwe Limited au Partnership Company.

Wewe na Mwekezaji/Wawekezaji mtengeneze Kampuni, na wewe ukubali kuwa wazo lako na utaalam ugeuzwe kuwa asilimia fulani za hisa/umiliki huku ukikubali kuwa Mtendakazi wa kujitolea mpaka muanze kutengeneza faida.
Labda utapewa 20%, 30% au vyovyote mtakavyo kubaliana. Wewe utakuwa na mandate ya kusimamia biashara (Mkurugenzi Mtendaji) na mwekezaji/wawekezaji watakuwa Non Acting Directors.

Hii itamhakikishia Mwekezaji/ Wawekezaji wa wazo lako usalama wa mali na pesa zao na faida na umiliki wa biashara. Hata kama usipokuwepo biashara itakuwa mahali salama, hata kama wewe utazingua basi wataweza kutoa kwenye utendaji na mali zao zikawa salama. Sio tuu upewe 50M kwa MPESA mkuu.

Kuna wewe, mwekezaji na biashara. Biashara sio wewe, biashara lazima iwe na hali ya kujitoa kutoka kwa mmiliki na ijitenge. Biashara lazima ijisimamie kwa risks, mali na faida na hapo ndipo kutakuwa na usalama wa uwekezaji. Yaani Mwekezaji atakuwa confident kuwekeza kwenye entity ambayo sio wewe.

There must be a legal and regulatory framework of the business. Ukisema tuu flani alete 50M tuwekeze, labda kama ni mhisani sio Investor.

Dunia ya watu werevu huendesha kitu kinaitwa "Equity Fund". Wazo lako linaweza vutia wawekezaji, na ndio maana leo unaona kuna firms kubwa zinakuwa na wazo, pesa zinatoka kwa wengine wenye lengo la kupata faida na wazo hilo.

Ili wazo lipate Wawekezaji, lazima liwe na ubunifu/innovative, linaweza kukua ( Scalable and replication), liwe endelevu na liwe katika teknolojia inayokuwa kwa muda huo. Linaweza kuwa na risk kubwa ila zinazoweza kusimamiwa.

Mimi binafsi nilipata fedha kwa namna hiyo, nakumbuka nilipokuyana na wawekezaji, waliniuliza maswali machache sana.

How innovative is your enterprise?
What are the potential risks and how will you manage it?
Explain your 3P's (People, Process and Products).
How will you scale-up this venture?

15 minutes zilitosha mimi kupata Mwekezaji wa wazo langu kwenye la Fin-tech. Leo sipo kwenye usimamizi ila ni Co-founder and Co-investor. Life goes on.


Kila la kheri.
 
Hivi ndio lengo la wazo lenyewe hapa mkuu umenipa conclusion ya nini kifanyike muwekezaji akishapatikana Mimi niliweka km utangulizi kujua nini kusudio inamaana anapotokea mtu wa kuhitaji kuwekeza inamaana lazima tufanye kitu legal kama ulivoshauri na hii kitu Mimi ndio msingi mana nilishakuwa na partner nikaona nilikosea wapi na yeye alikosea wapi hivo kwa hii issue lazima hii kitu izingatiwe especially kisheria kama ulivoshauri 🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…