NAOMBENI MNISAIDIE KIDOGO MCHANGO WA MAWAZOYENU!
Mm ni kijana mwenye umri wa miaka 22! Niko chuo mwaka wa pili, nasomea ualimu wa math & physics.
Baada ya kukusanya pesa kidogo kutoka kwenye boom takribani 1M mpaka sasa, hivyo nahitaji nijiengue kutoka kwenye elimu niwe mkulima wa mazao ya mpunga na mahindi.
WENYE UELEWA MNISAIDIE TAFADHARI ILA MSINITUKANE.
Mimi ni Mwalimu mwenzio tena Arts nimemaliza miaka michache ilopita.
Ushauri wangu ,maliza shule Kwanza Mimi nimepitia huko pia huwezi kupambania Elimu zaidi miaka 15 kisha uishie njiani eti ukaanze kulima Mafanikio hayako hivyo fanya jambo kwanza likamilishe unaweza usione matunda yake Leo au mapema lakini ipo siku Elimu itakulipa.
Nakuhakikishia pamoja na changamoto za soko la ajira bado Elimu inabaki kuwa mkombozi kwa watu tunaotoka kaya Maskini.
Hiyo Milioni iweke bajeti vizuri badala ya kulima kama unatoka vijjijini nunua mazao au nunua mbuzi kadhaa weka chukua nyingine jibajeti itumie kula vizuri soma vizuri hakuna haja ya kujitesa Huwa tunatafuta maisha huku tunaishi ,usitafute maisha ukasahau kuishia.
Naamini umenielewa.
Omba Mungu pia akupe hekima.