Nahitaji nijiengue kutoka kwenye elimu niwe mkulima wa mazao ya mpunga na mahindi

Upo sawa,, hujakosea ata.
 
Elimu kwanza pesa inatafutwa pesa huisha pesa inamajanga mengi
 
Kama masomo hayakupi shida sana jitaidi umalize chuo brother muhimu sana.. Jitahidi ujiongeze na biashara ambazo unaweza kufanya huku unasoma zitakusaidia..

Kama wewe ni mkaksi kimtindo wakopeshe wanafunzi wenzako kipindi boomlinakaribia kutoka wiki mbili tatu kabla hivi halafu likitoka wanakulipa Elfu 10 kwa 13, Hamsini kwa sitini na tano.

Kama unajua kudai vizuri hii inaweza kuwa biashara lakini pia kua mwangalifu unaweza ukatapeliwa hela yako yote... yote kwa yote tafuta biashara ambayo unaweza kuifanya ukiwa chuo na ukomae nayo..
 
Asante developer,, kinachonikatisha tamaa mzee wangu mdogo ni mwalimu ila cha ajabu hawezi ata kuhudumia familia yake chakula tu shida.
 
Hongera kwakuwa na SHAHUKU KUBWA ya mafanikio.
NB:Inaonekana ujawahi shika pesa nyingi (1,000,000 ndiyo ilikuwa ndoto yako),jipongeze kwa kutimiza lengo.

Wazo la kilimo ni sahihi kabisa. Aliyekushauri muulize
ilimchukua muda gani kufanikiwa?,muulize kuhusu changamoto zaidi kuliko faida!!!

Usiache shule kwa kutumia hisia na uthubutu,shirikisha pia akili (logic)

MUHIMU:Endelea kula Mihogo,jitese km vile huna pesa. Tunza sana ulichonacho (1,000,000 & Elimu).
"MSOMI ANAWEZA KUWA MWALIMU NA KUWA MKULIMA,ILA MKULIMA ANAWEZA KUWA MKULIMA TU"
 
Asante kaka,, ila duuuh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…