Nahitaji partner kwenye mradi wa ufugaji kuku wa nyama (broiler)

Wacha kupotosha umma hakuna broiler anaeuzwa baada ya wiki mbili
 
Kwenye chakula si chini ya elfu sitini mfuko, kwa kuku 2000 wakienda vizuri wanakula mifuko si chini ya 64, chukua 64000×64, ni Zaid ya 3M, acha kufurahisha watu na mahesabu ya haraka haraka, alafu wasipoenda vizuri utalisha chakula hadi uchizike, means wanaweza kula mifuko 80+ sasa chukua 60000 uzidishe kwa 80,

Nachotaka kusema ni kwamba biashara ya broiler ni nzuri na inahela lkn inahitaji pia mtaji wa kutosha uwe na hela ya kutosha ya chakula na dawa,

Hapo ukichelewa tu kuwapa dawa, nakwambia unaweza okota kuku nusu banda
 
Msameheni huyu kachizika [emoji1787][emoji1787]
 
Kwenye ujenzi wa mabanda umechemka ndugu yangu.kwa kawaida banda la kuku linatakiwa liwe na Kazi mbili tu zA tofali
 
kuku 2000 hawawezi kula viroba 30, kuku mmoja mpake awe wa kuuza anakula kilo 2.8-35, weka tu 3kg mara kuku 2000 ni kilo 6000, kiroba kimoja ni kilo 50, so hapo ni viroba 120 zidisha na bei ya chakula 65,000 wastani pamoja na usafiri = 7,800,000 hujaweka bei ya mtunzaji, Mbwa lazima uwe naye na pia maji utapataje lazima uwe na pump (umeme+mafuta, kuku 400 wanakunywa lita 100-140 za maji safi) na pia 10% ya kuku tegemea watakufa au kudumaa au watachelewea kufikia angalau kilo 1. kuna kazi nyingine ngumu sana ya kunyonyoa, usikubali wanyonyoaji waondoke na vichwa, miguu, utumbo nafirigisi bora uwalipe sh100-200 kwa kila kuku. LAZIMA UWE NA FRIGI KUBWA

Ki uhalisia biashara ya kuku wakati huu utalii umepungua huwezi pata faida kwenye nyama tu kwa bei ya 6500 lazima iwe juu ya hapo, faida utaipata kama utaweza kupata mnunuzi mzuri wa vichwa, firigisi(gizard), miguu na utumbo na vyote uza si chini ya sh 1000 hapo utapata sh2,000,000 na labda itaziba hasara ya kuku au kuongezea faida kidogo ya nyama ya kuku. hii biashara ya vichwa, utumbo, gizzard na miguu nenda soko koo na soko mjingajinga utapata wamama wanaipenda sana, kaa na namba zao za simu na uwe unawapa taarifa mapema siku ukichinja.
 
Kuku 2000 wanakula mifuko 60 kwa wiki 4

Lakini pia bado unafurahisha sana, yaani operating costs unazopiga wewe ni chakula na dawa tu halafua una calculate na kupata faida

Labour?
Maji?
Feed transport?
Mortality?
Security?
Deliveries?
Management?
Market delay?

Hivyo vyote kwenye project yako havipo
Trust me, unafanya biashara ya kwenye makaratasi na haitokufiksha popote

Nina uzoefu katika biashara hiyo, ukihitaji masaada kimawazo nirudie nitakusaidi free of chaege, achana na broiler farming unless una contract na mnunuzi
 
Reactions: apk
Hapo kwenye 2M + 1.9M =4m sijaelewa ni hesabu za darasa la ngapi.


Kule juu umesema kuna 4milion ambayo ni manunuzi ya vifaranga. Haya hiyo 2 milioni na 1.9 milioni ni kitu gani tena ambacho kimekuja kuwa sawa na 4milion?!

Jambo jingine.... Wewe hiyo 50% by 50% share ya mtaji na mapato umetumia vigezo gani king'amua hiyo partnership?!

Hebu fafanua, banda lako hapo lina monetary value ipi, wafanyakazi au wasimamizi...

Yaaani wewe katika hiyo 50%share umejievaluate vipi. It seems umekwama kifedha na upo desperate na mtaji wa pesa zaidi.

Na haujaweza kujua thamani ya pesa ilivyokubwa katika biashara yako hiyo. Nakushauri uje kivingine.....

Ikitokea loss jua kitakachopotea ni pesa ila sio mabanda wala hivyo vyombo vya kuku au wewe utakaekuwa una manage biashara.

Nadhani hii biashara imekaa ki Marger zaidi au ki acquisition. Yaani aje mtu na milioni nane zake hapo kisha mkae meza kuu mpange namna ya kuifanya biashara na yeye ajue ata profit wapi....
 
Hayo mabanda Mbona kama yameziribwa sana, kipindi joto likiwa kali mnafanyaje?
Hamna mabanda hapo. Banda la kuku linajitaji mzunguko wa hewa na yeye amejenga kama godown. Ugonjwa ukiingia hapo say kuharisha haponi hata kuku mmoja.

Pia issue ya madawa ame underrate sana. Broilers wana chanjo za lazima achilia mbali wakiumwa. Nina uzoefu wa ufugaji mwaka wa 15 sasa na nazijua changamoto zote
 
Mmhhh!!!,Mambo ya kushare kwenye miradi kuna changamoto kubwa Sana.
 
Kuku wa nyama sio mchezo mimi Sahiv nimepumzika kidogo, maana hii. Kitu ni pasua kichwa
 
Wapi huko unauza broiler kwa 6500??.....sana sana bei kubwa utakayouza ni shs 6000. Chakula mfuko ni 61,000 - 64,000 per 50kg bag.
 
Hao vigaranga 2000 unawapata wapi walivyo adimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…