Nahitaji partner kwenye mradi wa ufugaji kuku wa nyama (broiler)

Hesabu za kwenye makaratasi ingia ulingoni uicheze ngoma
 
Mabanda ya kuku dirisha linatakiwa lianzie kwenye kozi tatu ama nne kutoka kwenye msingi ili kuruhusu hewa ya kutosha na mwanga.

Picha ulizo post alifai kuwa banda la kuku tena kwa hidadi kubwa kama hiyo uliyosema.
 
Mkuu si vema kuongea kama huna data kamili. Unaweza kuwa na nia nzuri lakini ukatfsiriwa vibaya kutoka na aina ya data na information unazozileta humu ndani. Nitakusaidia kama ifuatavyo kutokana na ujuzi wangu,

Kwanza, nimepitia banda lako na nikushauri kitaalamu hilo banda halifai kufugia broiler, usijaribu hata kidogo maana si banda bora. Umejenga kama store ya kuifadhia mizigo

Pili, gharama ulizoainisha ni za kufikirika zaidi kwa wastani wa kawaida na ndipo hesabu zinavyopigwa ni kwamba

Kuku 2000 watatumia Mifuko 80
ambapo finisher ni 40bags, grower 20 bags na starter ni 20bags. Kwa chakula bora bei za starter mpaka finisher zina range kati ya TZS 60000 Mpaka TZS 63000 kwa sasa.

Kuku elfu mbili, madawa na Vitamins kadiri TZS 350,000.00, Hapo bado kuna gharama nyingine ndogo ndogo kama matandiko, umeme, maji n.k

Kwa kuku 2000 tu ili uwe safe side baada ya matengenezo uwe na cash inayoingia kwenye operation isiyopungua 10Mil.
 
Kuku 2000
Starter 20 @ 63000= 126000
Glower 40@61000= 2440000
Finisher 20@60000= 1200000
Chanjo 10000
Madawa 300000
Ume/joto 300000
Matandiko 100000
Maji 100000
Hiyo gharama halo juu ni 6M jumlisha vifaranga 4M jumla mkuu ni 10M
Mauzo
Kuku mmoja sasa ni 6000 × 2000= 1200000 faida ni 2M over
Nasema uongo ndugu zangu
 
Banda lako halina sifa ya kuwa banda la kuku. Pia mahesabu yako kinadharia zaidi hayana uhalisia.
 
Hapo umepiga mahesabu as if mortality rate ni 0%, lakini nikiona banda la huyo ndugu hicho kitu hakipo...
 
Hapo kwenye starter naona hesabu sio sawa
Pia bioi gharama za mtumishi, usafiri na hasara kwa watako kufa?
 
Faida mnayogawana 50% ni baada ya partner wako kutoa cost ya mtaji na running costs?
 
Aisee...wadau msameheni hakujua jf nizaidi ya anavyo elewa.mleta uzi wanakusubilia huku....
 
Mbona umefanya UJANJA UJANJA kwenye hizo hesabu zako? Bei ya kununulia vifaranga 2,000 ni 4m na ukijumlisha na gharama za chakula 1.9M, italeta jumla ya takribani 6M.
Mauzo ya 13,000,000 ukitoa 6,000,000 itabaki 7,000,000 tu. Iwapo mtagawana 50% kwa 50% yeye ataambulia 3,500,000/= tu.
Huoni kama atakuwa amewekeza kwenye UPUMBAVU? Wajinga ndio waliwao.
 
Kuku wanaanza kuuzwa baada ya wiki 4 mkuu then mabanda yako hayana ubora wakutosha madirisha madogo, alaf kwa bei ya shamba ni 6000 sio 6500 then soko la unalo la uhakika wa kuwa toa hao kuku kwa pamoja maana ikifika muda wakutoka hawajatoka unaanza kula hasara
 

Huyu jamaa hana experiences ya kuwa fuga au anafuga kienyeji kama anakuambia kuku anatolewa wiki mbil au tatu , huo si uongo wa wawazi kabsa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…