Nahitaji ushauri kwa mtaji wa 40 milionI

Nahitaji ushauri kwa mtaji wa 40 milionI

Millifire69

Senior Member
Joined
Jul 8, 2021
Posts
145
Reaction score
149
Habari za muda huu, Mimi ni kijana wa miaka 20, hivi karibuni ninatarajia kupokea 40mil, je ni biashara gani ya uhakika naweza kuifanya yenye pesa.

Mimi binafsi sipendelei maduka kabisa wala sifikirii, Ila nilikuwa nawaza kununua coaster hata kama used kwa mtu, nimpe mtu afanyie kazi kwa siku iwe inakuja atleats 70k huku nikiendelea na chuo.

Nawakaribisha mnipe mawazo yenu. Asante
 
Nunua ng'ombe 80 wakati wa kiangazi kama kambako na Maksai chagua zile zenye miili mikubwa let say 400,000 × 80 = 32,000,000.

Kanunulie huko minada ya Kondoa, Singida na Dodoma than tafuta eneo Morogoro hata heka 10 let say kila 200,000 × 10 = 2,000,000 weka budget za Pumba via mashudu plus malipo kwa wachungaji, Dokta na usafirishaji weka 4,000,000 Jumla hapo 32,000,000 + 2,000,000 + 4,000,000 = 38,000,000 Baada ya miezi 3 zikinenepa unauza 750,000 × 80 = 60,000,000 kupanga nikuchagua [emoji3][emoji24]
 
Hongera kuwa na wazo la kuinvest ukiwa shuleni.

Biashara ya usafirishaji ni risk sana kupoteza mtaji. Nina uzoefu kwenye hili

Kama utaweza nenda uweke hizo hela benki kwenye fixed deposit account wakati ukiendelea na masomo, na kiasi kidogo maybe 5M nenda uwekeze UTT ili uewe unazungusha kupata hela ya kujikimu.

Jitahidi kukwepa vishawishi vya makundi hapo chuoni ili uje uhitimu ukiwa salama kiafya (afya ya akili na mwili), kwani una nafasi kubwa ya kuja kufanikiwa as tayari una mtaji wa kuanzisha safari yako ya mafanikio.

Kila la kheri.
 
Hapana, lazima nisikilize kwa sababu haya mambo ukileta ujuaji hela yote itapukutika...

Fungua kituo cha polisi ajiri migambo wawili, anza na vibaka watatu na wafanye doria kwenye vilabu vya pombe lazima mtapata wahalifu wengi. Mkiwakamata lazima watoe pesa, kuingia kituoni bure lakini kutoka na pesa! Ndani ya week mna pesa za kutosha mnafunga kituo, mnakihamisha mitaa mingine ndani ya mwezi hiyo 40million itakuwa imeongezeka sasa njoo tufanye biashara ya soya [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hongera kuwa na wazo la kuinvest ukiwa shuleni.

Biashara ya usafirishaji ni risk sana kupoteza mtaji. Nina uzoefu kwenye hili

Kama utaweza nenda uweke hizo hela benki kwenye fixed deposit account wakati ukiendelea na masomo, na kiasi kidogo maybe 5M nenda uwekeze UTT ili uewe unazungusha kupata hela ya kujikimu.

Jitahidi kukwepa vishawishi vya makundi hapo chuoni ili uje uhitimu ukiwa salama kiafya (afya ya akili na mwili), kwani una nafasi kubwa ya kuja kufanikiwa as tayari una mtaji wa kuanzisha safari yako ya mafanikio.

Kila la kheri.
Mungu akujalie..🙏 Asante sana kwa ushauri mzuri
 
Wewe huchelewi kumwambia Dada wa watu akupeleke Zanzibar mkainjoi maisha 😅😅😅
Ah wee maenye natamani kweli kwenda hotel verde ila sasa chumba laki nne unusu kwa siku sii balaa hilo.
On serious note though 10mil wat business can i do ambayo 30k kwa siku sikosi
 
Back
Top Bottom