Nahitaji ushauri wenu kuhusu uhusiano wangu na mke wangu

Nahitaji ushauri wenu kuhusu uhusiano wangu na mke wangu

Ni wazi kuwa bado ana some feelings na Ex wake,
Ni suala la wewe kufanya tathmini,
ukiunganisha na matukio mengine pamoja na hali ya sasa ya mahusiano yenu,
Utakayoyabaini yakusaidie kujua nafasi yako
Nafasi ya kumsikiliza ni ya muhimu sana, hupaswi kufikia conclusion kwa kusikiliza maoni ya nje, bila kumpa muhusika nafasi...na uamuzi wa mwisho uwe ni wako peke yako, maana wewe ndiyo unajifahamu vizuri
 
Nina jambo zito ambalo limenifanya niwe na wasiwasi mwingi, na nataka kupata mawazo ya watu wengine ili nijue ni vipi niendelee.

Hivi karibuni, nilikuwa nikichunguza simu ya mke wangu na kugundua kwamba anayo akaunti nyingine ya TikTok ambayo haina picha wala followers. Nilichokutana nacho kwenye sehemu ya search ya akaunti hiyo kiliashiria kuwa bado anahusiana na ex wake kwa namna fulani, na hii ilinifanya niwe na maswali mengi. Hii imeleta wasiwasi kwangu na kujua kama bado anamhisi ex wake au kama kuna kitu ambacho hajaniambia.

Nashindwa kujua ni hatua gani niichukue. Nataka kujua kama ni vyema kumwambia mke wangu hili na tuzungumze, au kama inafaa kuwaachana na kutafuta mtu mwingine kwa kuwa nampenda, lakini najihisi kama sina uhakika tena na hali yetu.

Je, ni vema kumwambia mke wangu hisia zangu au ni bora nimpe uhuru ili tuendelee na maisha yetu kwa njia tofauti?

Ningependa sana kupata mawazo ya watu ambao wamepitia hali kama hii au wanaweza kutoa ushauri mzuri kuhusu namna ya kushughulikia jambo hili.


View attachment 3225775



View attachment 3225776
Umefanya jambo jema sana kuomba ushauri....!! Mimi nakupa ushauri ulio gawanyika katika sehemu kuu 2
1. Mkeo mwache ila hakikisha unatupatia namba yake ya simu pamoja na handle yake ya iyo TikTok kwa maana kwamba tuweze kumliwaza pindi ambacho wewe umemwacha hii itamsaidia kupunguza maumivu ya kuachwa sio lazima uachane na mtu then ateseke kwa kizungu tunaita win - win situation


2. Mkeo usimwachie ila mtafutie nyumba ndogo hii itasaidia asijione keki, kwa maana kwamba kumuacha humuachi kwasababu bado unampenda ila kumpenda mkeo sio sababu ya kutowapenda wanawake wengine akiendelea kuleta kiburi unamuongezea nyumba ndogo nyingine zinakuwa 2 au tatu mpaka aache upumbavu wake ila wakati huu wote yeye ndo unayempa kipaumbele kama mke unayempenda

Unaonaje hapo?
 
Sijajua ni ganja za zaja usiku zinanifanya niwe hivi ama niaje
Ama shida sina D mbili?

Hapo amesaliti nini wakuu?
 
Ukipatwa ndiyo utajua inahuma kiasi gani usisubiri kupatwa muwahi ili mjue kila mtu ana hamsini zake au mnaweka mambo wazi mezani,ndoa sio rahisi bila kumuweka Mungu kama msimamizi wenu mkitumia akili zenu hamtoboi maana ndoa inapingwa sana na shetani
 
Ndoa ina miaka miwili nanusu
Tulijuana naye 2017 tukaoana 2022
Mke wangu miaka 27
So it means kuanzia 2017 ulikuwa upo nae kwenye mahusiano?

Najaribu kufikiria from 2017 to 2022 marriage, then from 2017, ,2022 up-to-date

Huyo ex ana kipi Cha upekee kiasi cha kushindwa kusahauliwa?

Je ex wake ndiye first man wake? Tho hii Haina maana sana!

Okay! Age ya mkeo nayo, kama kwa umri huo si wale wadada wenye hofu ya Mungu, watu wa maombi and mostly wenye Maarifa na upeo mkubwa wa kufikiri! Inaweza kuwa changamoto!

Kikubwa kaa nae chini kwa upendo mueleeze ulichokiona! Mueleze madhara ya yeye kufanya ivo juu ya ndoa yenu!

Read her mind, her spirit wakati ukiwa unaongea juu ya hili jambo!

Kama anajielewa ataacha na kubadilika ila ni wakina shwashwasu itakuwa ngumu
 
Haya mambo bwana....anyways mie sioni makasiriko ya nini mkeo kutaka kuwasiliana na ex wake....sii anataka kupasha kiporo tuu, she will still be ur wife na wewe una uhuru wakwenda pasha kiporo na ex wako pia
 
So it means kuanzia 2017 ulikuwa upo nae kwenye mahusiano?

Najaribu kufikiria from 2017 to 2022 marriage, then from 2017, ,2022 up-to-date

Huyo ex ana kipi Cha upekee kiasi cha kushindwa kusahauliwa?

Je ex wake ndiye first man wake? Tho hii Haina maana sana!

Okay! Age ya mkeo nayo, kama kwa umri huo si wale wadada wenye hofu ya Mungu, watu wa maombi and mostly wenye Maarifa na upeo mkubwa wa kufikiri! Inaweza kuwa changamoto!

Kikubwa kaa nae chini kwa upendo mueleeze ulichokiona! Mueleze madhara ya yeye kufanya ivo juu ya ndoa yenu!

Read her mind, her spirit wakati ukiwa unaongea juu ya hili jambo!

Kama anajielewa ataacha na kubadilika ila ni wakina shwashwasu itakuwa ngumu

Ex wangu niliyeachana nae mwanzoni mwa 2016 lakini hadi muda huu sijamsahau, hana kitu cha upekee
 
Ndoa sio kubeti kaka.. Wewe ndo mwenye maisha yako na mke wako. Ukisikiliza ushauri wa kila mtu utazidi kuchanganyikiwa mana kila mmoja ana akili yake na maamuzi yake, Labda ungetafuta mtu mmoja unayemwamini ndo umuombe ushauri kuliko kuja kuomba huku mana kuna wengine watakukejeli na vtu kama izo ambavyo bado vitakutia stress.

Wewe ndo muamuzi wa mwisho wa maisha yenu kwenye ndoa yako.

SIMAMA KIUME AMUA KAMA MWANAUME UTIE HURUMA.🙋🏻‍♂️
 
Kutokana na hiyo history inaonesha binti anapitia mgogoro ndani ya nafsi yake kuhusu huyo mwamba [ex] n kama ex wake amerudi kwenye maisha yake kwa kasi na anajiuliza if its really ama sio.Ex akikaza anaweza kupewa nafasi😔😔 kama mume wake unabidi ukae nae mzungumze na umkanye akiendeleza mawasiliano au mazoea na ex mnaweza msifikie malengo kama wanandoa/wanafamilia sio lazima kumuonesha umeona kitu kwenye simu yake ila tafuta namna ajue anachokiwaza au kukifikiria sio sawa kwa mustakabali wa maisha yenu.
 
Back
Top Bottom