Naianza Safari ya kujenga na kuendesha Chuo cha Elimu ya Kati (Certificate na Diploma)

Druggist

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2010
Posts
439
Reaction score
528
Wakuu Habari za Majukumu.

Imekuwa ndoto yangu kuanzisha na Kuendesha Chuo cha Elimu ya Kati,kinachotoa Elimu ya stashahada na astashahada hasa kwenye Kada ya Afya.Tayari Nina Eneo la Kutosha Kujenga Majengo.Kwa ambao tayari wanaendesha hii Shughuli nini cha kuzingatia?

Sijawahi kuwa Mwalimu lakini Katika Utumishi wangu niliwahi kuwa mkaguzi wa Vyuo hivi kwa niaba ya NACTE na Mabaraza Kadhaa ya kitaaluma.Kwa ukaguzi huu ndipo nilivutiwa siku moja kuanzisha na kuendesha Chuo.

Karibuni hasa wale wazoefu wa Usimamizi wa Vyuo.
 
Una mtaji kiasi gani mkuu, lazima ujiandae kifedha
Nina Mtaji wa Ardhi,na pia technical knowhow.Majengo na Samani pia nahitaji Ninawazia.Uendeshaji ndiyo nitahitaji wabia.
 
Wazo zuri sana. Natamani pia kupata huo uzoefu.
 
Katika hivi vyuo vya kati vya afya,kuna certificate?Mimi nikifikiri ni diploma tu.Kwa mfano ufamasia,wanasona certificate?Na ni miaka mingapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…