GE2025 Naibu Katibu Mkuu TEC, Padri Msaga: Tusipotenda Haki, Amani haiwezi kutawala kamwe

GE2025 Naibu Katibu Mkuu TEC, Padri Msaga: Tusipotenda Haki, Amani haiwezi kutawala kamwe

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Chesco Msaga, C.PP.S, leo Novemba 7, 2025 katika Ibada ya kuwaombea marehemu na majeruhi wote waliopata madhara katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, amesema, “Haki ndiyo huzaa amani. Tusipotenda haki, amani haiwezi kutawala kamwe.”

 
Kuskia kwa kenge mpaka damu itoke kwenye maskio
 
Ndiyo, hiyo ndiyo kauli sahihi iliyobeba ukweli sahihi

Popote palipo DHULUMA badala ya HAKI, hapana AMANI hapo

Viongozi wetu na machawa wao wanalikwepa mno kulitamka neno HAKI kwa sababu mioyo na nafsi zao zinawashitaki kwa kuwa zimejaa dhuluma.

Nilishangaa kweli jana Mch Lusekelo a.k.a Mzee wa Upako analaumu wananchi hususani vijana waliouwawa kwa kupigwa risasi na polisi kwa kusema "mmepigwa risasi mkafa kwa kuwa mnadai HAKI badala ya kuitafuta AMANIkwanza!!"

Huyo ni mchungaji.

Ni mchungaji wa kanisa la Yesu Kristo aliyesahau kuwa Biblia - Neno la Mungu inasema "YEYE MUNGU NDIYE HAKI" na "AMANI ni tunda la HAKI"

Ukisigina haki za watu tu, Amani inatoweka mahali hapo na kinachofuata ni vurugu na machafuko. Ndiyo yaliyotokea tangu tarehe 29/10 na yataendelea kama hatutakuwa na hekima na busara kuutambua ukweli huu!;
 
Back
Top Bottom