johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Katika hali isiyotarajiwa, Naibu wa Kenya Rais Rigathi Gachagua ameripotiwa kuzidiwa na kupelekwa hospitalini zikiwa zimebaki dakika chache kabla ya kutoa ushahidi wake.
Wakili wake, Paul Muite, aliwaambia Maseneta kuwa Gachagua alizidiwa baada ya chakula cha mchana wakati akisubiri kesi ya kumwondoa madarakani iendelee .
Ikumbukwe kuwa leo, Maseneta walitarajiwa kupiga kura juu ya mashtaka 11 yanayomkabili Gachagua.
Muite alisema, “Ukweli mchungu ni kwamba Naibu Rais wa Jamhuri ya Kenya ameugua sana, na anapokea matibabu hospitalini."
Muite hakufichua ni hospitali gani Naibu Rais amepelekwa wala aina ya ugonjwa unaomsumbua.
Gachagua alitarajiwa kutoa ushahidi wake mwenyewe katika kesi hiyo ya kumvua madaraka yake kama Naibu Rais
Spika Kingi alisema,
“DP alitarajiwa kutoa ushahidi. Nilitangaza mpango uliotakiwa kufanyika mchana, na nikaeleza kuwa tutautekeleza mpango kwa umakini ili tumalize jambo hilo leo. Wakili Paul Muite alisema hawezi kumfikia mteja wake, lakini hilo si jukumu la Bunge. Seneti inamngoja Naibu Rais, hakuna Seneta mwingine atakayechukua nafasi hiyo."
Source: Nation Africa
Pia, soma: Yanayojiri katika Kesi ya kumuondoa Madarakani Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua leo Oktoba 17, 2024