Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo ajibu sakata la Bandari ya Bagamoyo. Asema Serikali haijaingia makubaliano yoyote ya uwekezaji
Soma: Ubalozi Wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Watoa Maelezo ya Kina juu ya Upotoshaji unaoendelea Mitandaoni
"Serikali ipo katika hatua mbalimbali za kutekeleza program ya ujenzi wa eneo maalum la kiuchumi la eneo la Bagamoyo na hili ni moja ya miradi 17 ya kielelezo iliyopo katika mpango wa tatu wa maendeleo ya miaka mitano 2021/22-2025/26"
"Pamoja na mambo mengine eneo hili linahusisha ujenzi wa miradi mingi lakini moja ni ujenzi wa Bandari, Kongani za Viwanda, Kongani za TEHAMA, Ukanda huru wa biashara na kituo cha Reli. Kwahiyo sio mradi mmoja na ndio maana tunaita program"
"Utekelezaji wa program hii utatekelezwa na sekta binafsi kwakushirikiana na serikali kupitia mpango wa ubia katika sekta binafsi na sekta ya umma yaani Public–private partnership (PPP)"
"Wadau mbalimbali kutoka ndani na nje wameonyesha nia ya kuwekeza, wadau hawa wako katika hatua mbalimbali za mazungumza na taasisi husika. Serikali haijaingia makubaliano yoyote na mwekezaji yoyote kwasasa, wala hatuna mkataba na mwekezaji yoyote katika miradi ya Bagamoyo ikiwemo niliyoitaja wa Bandari"
Soma: Tetesi: - Saudi Arabia yapewa haki ya umiliki na uendeshaji wa bandari ya Bagamoyo kama sehemu ya mradi wa East Gate
========================================================
"Serikali ipo katika hatua mbalimbali za kutekeleza program ya ujenzi wa eneo maalum la kiuchumi la eneo la Bagamoyo na hili ni moja ya miradi 17 ya kielelezo iliyopo katika mpango wa tatu wa maendeleo ya miaka mitano 2021/22-2025/26"
"Pamoja na mambo mengine eneo hili linahusisha ujenzi wa miradi mingi lakini moja ni ujenzi wa Bandari, Kongani za Viwanda, Kongani za TEHAMA, Ukanda huru wa biashara na kituo cha Reli. Kwahiyo sio mradi mmoja na ndio maana tunaita program"
"Utekelezaji wa program hii utatekelezwa na sekta binafsi kwakushirikiana na serikali kupitia mpango wa ubia katika sekta binafsi na sekta ya umma yaani Public–private partnership (PPP)"
"Wadau mbalimbali kutoka ndani na nje wameonyesha nia ya kuwekeza, wadau hawa wako katika hatua mbalimbali za mazungumza na taasisi husika. Serikali haijaingia makubaliano yoyote na mwekezaji yoyote kwasasa, wala hatuna mkataba na mwekezaji yoyote katika miradi ya Bagamoyo ikiwemo niliyoitaja wa Bandari"
========================================================
TAMKO LA SERIKALI KUHUSU UENDELEZAJI WA ENEO MAALUM LA KIUCHUMI LA BAGAMOYO (BAGAMOYO SPECIAL ECONOMIC ZONE-BSEZ)