Naibu Spika Zungu: Bodaboda wanakatisha tamaa, wasimamishwe

Naibu Spika Zungu: Bodaboda wanakatisha tamaa, wasimamishwe

Ukitaka kujua shughuli yao mida ya jioni pale mataa ya Kariakoo wanapovuka kuelekea Mbagala. Wee..

Yaani wanakuwaga kama nyuki.
 
Zungu anazungumzia ishu ya boda boda huku hawana mbadala hata wa kushusha kodi za Bajaji au magari madogo...
 
Ila kiukweli kunahitajika mkakati madhubuti kwa hawa vijana. Aisee ajali ni nyingi. Halafu wengi wao hawafuati kabisa sheria za usalama barabarani.
Wanazifata wapi? Wanazijua hata!? Mtu anatoka kuendesha baiskeli,akijua tu kubadiri gia,anaingia barabarani.
Siku kukiwa na utaratibu wa kupata leseni halali,hayo yote yataisha.
 
"Suala la bodaboda ni kero kubwa sana na hasa katika utumiaji wa sheria za barabara, mimi ni mtetetezi mkubwa sana wa bodaboda lakini matumizi yao kwenye barabara yanakatisha tamaa lazima muwe na mkakati maalum wa kudhibiti ajali wanazozifanya na lazima muwe na sheria kali za kuwadhibiti na hata kuwasimamisha, sababu ukienda MOI sasa hivi asilimia 90 ni vijana," - Mussa Azan Zungu

View attachment 2894963

Credit-EastAfricaTv
Angesema Bajaj ningemwelewa.
 
Kwa nchi kama Tz hili jambo haliwezekaniki, kabisa nchi iliyojaa rushwa na siasa za kijinga, haiwezi kutokea, bodaboda kufata, sheria au kuwatoa hiyo haitatokea kwa nchi, Tanzania.
 
Kwa nchi kama Tz, hili jambo wala haliwezekaniki, kabisa kwa nchi iliyojaa rushwa na siasa za kijinga, bodaboda haitatokea kufata, sheria au kuwatoa, hiyo tutengemee kuwa itabaki hivyovyo tu, hata kama utathubutu kuwatoa, itakua taaruki kubwa sana, nchini na maandamano ambayo yataishinda serikali, na watatokea wanasiasa kuwatetea huku, jicho likiwa kwenye kula, na malizia sasa, kwa kusema kwa nchi kama, Tanzania, haiwezekaniki??
 
Mdogo mdogo ile kauli ya Mh Lema naona imeanza kuwaingia
 
Iwe akifanya kosa auliwe hapohapo tu
 
Kwanza ni bodaboda wangapi wana leseni za udereva, hilo tu serikali imeshindwa kufuatilia. Hii nchi yetu kila kitu kinajiendea tu.

Vijana wengi katika hii ahira wamekuwa wanywa smart gin, hali inazidi kuwa mbaya.
Tufanyeje sasa mkuu!?
 
Huyo hata aseme nn mm simuelewi maana ndo kaleta ma upuuzi ya tozo sasa hivi analeta swala la boda boda huku nae ubunge hataki kuachia vijana. Wakati wako busy kutunga sheria za kuwapa maisha wao na familia zao..kuna wavunja sheria kama ccm na viongozi..mamaaaaaaaeee
 
images.jpg


Hakika wanakatisha tamaa...


Cc: Mahondaw
 
Unawavunjia heshima ni maafisa wasafirishaji
 
"Suala la bodaboda ni kero kubwa sana na hasa katika utumiaji wa sheria za barabara, mimi ni mtetetezi mkubwa sana wa bodaboda lakini matumizi yao kwenye barabara yanakatisha tamaa lazima muwe na mkakati maalum wa kudhibiti ajali wanazozifanya na lazima muwe na sheria kali za kuwadhibiti na hata kuwasimamisha, sababu ukienda MOI sasa hivi asilimia 90 ni vijana," - Mussa Azan Zungu

View attachment 2894963

Credit-EastAfricaTv
Nendeni Rwanda tu hapo mkaone bodaboda wanavyofuata sheria ,mavazi yao ,kofia zao n.k ni suala la lazima sio ombi kutii sheria

Nilipanda bodaboda katikati ya mjii lakini nilijihis salama zaidi kuliko hata ningekuwa mkoani vijini nchini kwetu
 
Fata Sheria Boda Boda wewe
Sijawahi kuwa bodaboda
Hivi unajua kuwa wanaoongoza kuvunja sheria za barabarani ni hao viongozi na watu wa usalama yeye amewaona boda tu eti

Vp umewahi kufika ilala soko la mazao msimu wa mvua? au barabara ya uhuru sijui pale njia daladala za temeke zinapopakia kuja mpaka ilala kwenyewe?
au kuanzia kamata kuja kkoo?
Au kkoo nzima inavyonuka vinyesi na Chemba zinazotoa vinyesi vibichi
Huyo anaongea nini sasa
Ameshiba maharage akae kimya hajui lolote
 
Too late
Na sasa hivi ndio hamuwawezi kabisaaaaa
Yaani mkijipendekeza tu na vita inaamka na kuamka, hawa jamaa wa bodadaboda na bajaji wana nguvu kuliko mnavyodhani,

Hapa mtaani kwetu kila siku polisi, polisi kama polisi wanapigwa na wanasepa
Itakuja kuwa mgambo?

Toooooo late
 
Back
Top Bottom