Naibu Spika Zungu: Bodaboda wanakatisha tamaa, wasimamishwe

Naibu Spika Zungu: Bodaboda wanakatisha tamaa, wasimamishwe

Mkuu raraa,

kuondoka au kusimamisha pikipiki ni jambo ambalo haliwezekani kwa namna yoyote ile.

Hapo inaonyesha ni jinsi gani serikali ilivyo mbovu katika kusimamia sheria.

Wanetanguliza rushwa mbele, na rushwa hutengeneza upofu na kushindwa kuelewa ni wapi pakusimama.

Kusimamisha bodaboda, tutegemee panya road wakutosha, wavuta bangi wa kutosha, mauaji ya kutosha.hata baadhi ya biashara hasa zinazohusika na spea za pikipiki kudorora.

Zitengenezwe sheria kali za kudhibiti vijana,kama pale airport mataa ni hatari sana, na unakuta bodaboda anapita na trafiki anamuangalia tu.

shida ni hii hapa “nani atasimamia hizo sheria kwenye nchi hii ambayo neno kila mtu anakula kwa Urefu wa kamba yake limetawala?

Polisi wa barabarani wanaenda mpaka machimbo ya mchanga kukamata malori na kuwatishia kuwafungulia kesi hawana vibali!

matrafki hawa ambao wanashindana kujenga majumba kwa pesa za dhuruma nani wakusimama kupunguza vijana hawa wanavyopoteza maisha na wengine ulemavu?

Kama zikitengenezwa sheria kali za kukamata pikipiki na faini kali Hakika tatizo litapungua kwa kiasi kikubwa.
Kuliko kuendelea kupokea elfu 5 za vijana na wakiwaacha wafanye wanayofanya.
Nakuelewa Lakin mazingira ya usafiri wa bodaboda ndo unafanya I've ngumu kwa askari kuweza kupambana nao tofauti na gari,mfano hapo mataa ya airport umemsimamisha bodabodq amepitiliza unamkamata vipi?? Ili umkimbize na ww itabidi uv7nje sheria uchukue pkpk nyingine uende kasi zaidi yake! Na kwq mazingira ya sasa ya dar utakimbizana na bodaboda ngp??
 
Kwa hili namuunga mkono mh Naibu Spika.

Boda Boda waliowengi wapo rough sana katika uendeshaji wao na kibaya zaidi hawafuati sheria za barabarani.

Ajali zimekuwa nyingi tena wakati mwingine wanasababishiana boda boda kwa boda boda yaani unakuta mwingine anaendesha kistaarabu kisha mwingine tena bila tahadhari anakwenda kama mwendawazimu na kuleta ajali.

Wengi ni vijana wadogo na wahuni wanaotumia pombe, Sigara, bangi na vilevi vingine.

Ni watu wasiofuata utaratibu kabisa na sasa hivi ndiyo zinazidi kuongezeka maana boda boda kwa sasa imekuwa kimbilio la wengi.

Najaribu kutafakari baada ya miaka 15 hii hali ikiendelea sipati picha idadi ya hizo boda boda humo barabarani.

Sasa hivi hata kama una mtoto kumtuma hata dukani unapata mashaka makubwa, kila leo Ajali watoto wa shule za msingi wanagongwa na hizi boda boda.
Wiki iliyopita boda mmoja kajisababishia ajali kipumbavu sana, ilikuwa hivi; ameendesha pikipiki akiwa kalala sio usingizi yani kama ile michezo amelalia pikipiki miguu iko kwenye kiti kile cha abiria, kifua kalaza kwenye tank ya mafuta.

Endapo uko mbele yake kwa umbali kidogo unaweza sema ile pikipiki haina mwendeshaji kumbe yupo ila kailalia, mimi amenipita kama kishada naenda kama mita 150 nakuta kundi la watu kumbe boda amepiga chini tena kwenye jiwe pembeni mwa barabara kapasuka kichwani damu nyingi inamtoka na alikuwa design kazimia.

Hawa vijana wanahitaji sheria kali kudhibiti ajali, shida ni moja mfano kwenye baadhi ya miji askari wa usalama barabarani hawana time na boda hata kidogo, wao wako bize na magari sasa namna hii boda hawana cha kupoteza ni kumwaga moto matokeo yake ni ajali tena weekend ajali njenje.
 
Ila kiukweli kunahitajika mkakati madhubuti kwa hawa vijana. Aisee ajali ni nyingi. Halafu wengi wao hawafuati kabisa sheria za usalama barabarani.
Hawafuati mkuu tena wana ile tabia ya ku-over take upande wa kushoto... Wewe umeconcentrate kulia mara boda unashangaa kapita speed tena upande aliopita sio sahihi sasa fikiria unapishana na gari kisha unatanua kidogo mara paap boda huyu!! Hawa vijana ni balaa
 
Nakuelewa Lakin mazingira ya usafiri wa bodaboda ndo unafanya I've ngumu kwa askari kuweza kupambana nao tofauti na gari,mfano hapo mataa ya airport umemsimamisha bodabodq amepitiliza unamkamata vipi?? Ili umkimbize na ww itabidi uv7nje sheria uchukue pkpk nyingine uende kasi zaidi yake! Na kwq mazingira ya sasa ya dar utakimbizana na bodaboda ngp??
Mkuu mliverpool,

Embu tufikirie kwamba kwa sasa tupo na tatizo kubwa la vijana wengi wa bodaboda kupoteza maisha, na wengine wengi kuishia ulemavu.

sababu bado miili yetu damu inachemka hivyo mara nyingi tunafanya vitu aggresive bila kufikiri matokeo yake yatakuwa vipi.

Mfano, sababu kuongea na vijana kwa semina bado ni jambo gumu na kila siku wanaona wenzao wanapotea lakini bado hawajifunzi.

Suluhisho kubwa ni kuweka sheria kali.

Kwanini sehemu ya mataa kama pale airport pasiwepo kamera za barabarani? Halafu katika vituo wakawepo trafiki pamoja na barrier ambazo zitakuwa zinafanya kazi kwa sababu maalumu ya vijana wanaovunja sheria.

Kama alikuwa anatokea mjini anakuja g/mboto trafiki wa airport watatoa taarifa kwenda kituo cha posta au njia panda segerea pamoja na kamera ambazo zitakuwa zimeshanasa aina ya pikipiki pamoja na namba za usajili wa pikipiki hiyo.

Kuwepo kwa Taa tumeshaona bado si suluhisho la vijana kutii, Kwanini wasiwepo trafiki ili polisi watapotoa taarifa kituo tukio lilipotokea kituo kinachofata Polisi wasogee barabarani na barrier zikishishushwa.

Kama Kutakuwa na consistency ya kipindi cha muda mrefu nina hakika tutapunguza vifo vya bodaboda.
 
"Suala la bodaboda ni kero kubwa sana na hasa katika utumiaji wa sheria za barabara, mimi ni mtetetezi mkubwa sana wa bodaboda lakini matumizi yao kwenye barabara yanakatisha tamaa lazima muwe na mkakati maalum wa kudhibiti ajali wanazozifanya na lazima muwe na sheria kali za kuwadhibiti na hata kuwasimamisha, sababu ukienda MOI sasa hivi asilimia 90 ni vijana," - Mussa Azan Zungu

View attachment 2894963

Credit-EastAfricaTv
Aliposema Lema aliitwa kila jina baya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom