Naibu Spika Zungu: Bodaboda wanakatisha tamaa, wasimamishwe

Nakuelewa Lakin mazingira ya usafiri wa bodaboda ndo unafanya I've ngumu kwa askari kuweza kupambana nao tofauti na gari,mfano hapo mataa ya airport umemsimamisha bodabodq amepitiliza unamkamata vipi?? Ili umkimbize na ww itabidi uv7nje sheria uchukue pkpk nyingine uende kasi zaidi yake! Na kwq mazingira ya sasa ya dar utakimbizana na bodaboda ngp??
 
Wiki iliyopita boda mmoja kajisababishia ajali kipumbavu sana, ilikuwa hivi; ameendesha pikipiki akiwa kalala sio usingizi yani kama ile michezo amelalia pikipiki miguu iko kwenye kiti kile cha abiria, kifua kalaza kwenye tank ya mafuta.

Endapo uko mbele yake kwa umbali kidogo unaweza sema ile pikipiki haina mwendeshaji kumbe yupo ila kailalia, mimi amenipita kama kishada naenda kama mita 150 nakuta kundi la watu kumbe boda amepiga chini tena kwenye jiwe pembeni mwa barabara kapasuka kichwani damu nyingi inamtoka na alikuwa design kazimia.

Hawa vijana wanahitaji sheria kali kudhibiti ajali, shida ni moja mfano kwenye baadhi ya miji askari wa usalama barabarani hawana time na boda hata kidogo, wao wako bize na magari sasa namna hii boda hawana cha kupoteza ni kumwaga moto matokeo yake ni ajali tena weekend ajali njenje.
 
Ila kiukweli kunahitajika mkakati madhubuti kwa hawa vijana. Aisee ajali ni nyingi. Halafu wengi wao hawafuati kabisa sheria za usalama barabarani.
Hawafuati mkuu tena wana ile tabia ya ku-over take upande wa kushoto... Wewe umeconcentrate kulia mara boda unashangaa kapita speed tena upande aliopita sio sahihi sasa fikiria unapishana na gari kisha unatanua kidogo mara paap boda huyu!! Hawa vijana ni balaa
 
Mkuu mliverpool,

Embu tufikirie kwamba kwa sasa tupo na tatizo kubwa la vijana wengi wa bodaboda kupoteza maisha, na wengine wengi kuishia ulemavu.

sababu bado miili yetu damu inachemka hivyo mara nyingi tunafanya vitu aggresive bila kufikiri matokeo yake yatakuwa vipi.

Mfano, sababu kuongea na vijana kwa semina bado ni jambo gumu na kila siku wanaona wenzao wanapotea lakini bado hawajifunzi.

Suluhisho kubwa ni kuweka sheria kali.

Kwanini sehemu ya mataa kama pale airport pasiwepo kamera za barabarani? Halafu katika vituo wakawepo trafiki pamoja na barrier ambazo zitakuwa zinafanya kazi kwa sababu maalumu ya vijana wanaovunja sheria.

Kama alikuwa anatokea mjini anakuja g/mboto trafiki wa airport watatoa taarifa kwenda kituo cha posta au njia panda segerea pamoja na kamera ambazo zitakuwa zimeshanasa aina ya pikipiki pamoja na namba za usajili wa pikipiki hiyo.

Kuwepo kwa Taa tumeshaona bado si suluhisho la vijana kutii, Kwanini wasiwepo trafiki ili polisi watapotoa taarifa kituo tukio lilipotokea kituo kinachofata Polisi wasogee barabarani na barrier zikishishushwa.

Kama Kutakuwa na consistency ya kipindi cha muda mrefu nina hakika tutapunguza vifo vya bodaboda.
 
Aliposema Lema aliitwa kila jina baya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…