Naibu Waziri aagiza ujenzi soko la kisasa Muleba kukamilika ndani ya miezi sita

Naibu Waziri aagiza ujenzi soko la kisasa Muleba kukamilika ndani ya miezi sita

jjackline

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
111
Reaction score
274

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Zainab Katimba amemwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, mkoani Kagera akamilishe haraka hatua za manunuzi na kupata mkandarasi wa ujenzi wa soko la kisasa la Muleba na kuhakikishe ujenzi unakamilika ndani ya miezi sita.

Katimba ameeleza hayo jana Jumapili Agosti 11, 2024 kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Tamisemi, Mohamed Mchengerwa kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi uliofanyika Muleba Mjini, wakati akijibu kero za wananchi.

“Ujenzi wa soko hilo upo hatua ya manunuzi na kupata mkandarasi, akipatikana mkandarasi inabidi ajenge ili wananchi waanze kutumia soko hili kwa maana lilikuwepo, lakini linaboreshwa. Kwa hatua hii naomba kumsisitiza mkurugenzi aharakishe taratibu za manunuzi na mkandarasi apatikane na ndani ya miezi sita ajenge soko hilo, ili wananchi waanze kulitumia kwa sababu fedha ipo Sh2 bilioni,”amesema.
Snapinsta.app_455021204_828009142794514_3718649502896886359_n_1080.jpg
 
soko gani linakamilika ndani ya miezi 6. hapa tarime soko lina miaka sita ,tunaona tu wamezungushia mabati
 
Back
Top Bottom