jogi
JF-Expert Member
- Sep 25, 2010
- 25,556
- 25,371
Ukiangalia kwenye profile yake ya Bunge inaonesha alisoma shule ya Msingi Makunda (sijui iko wapi? Singida ama Usukumani?), kuna yeyote anaijua shule hii vizuri? Kama yupo naomba aelekeze jinsi twaweza fikia mtu wa huko tupate uhakika zaidi, manake haya mambo bana kiasi yanasumbua unajua mtoto wa nyoka ni nyoka na kama ni kweli alinunua jina inabidi kiasi tuanze kufukunyua integrity yake ambayo watu tunaassume ipo safi. Unajua hata Mulugo - yule naibu waziri elimu, naye kimemtokea cha hivi hivi na ndiyo maana siku hizi anaonekana kunywea. Watu wa hivi ndiyo walikuwa wananyanganya watu haki zao za kusoma, ukizingatia zamani waliomaliza la saba ili kwenda Sekondari wanafunzi walikuwa WANACHAGULIWA baadhi tu ya waliofaulu. Ila pia hata mimi nimekuwa najiuliza sana huyu bana Nchemba mbona anaonekana mkomavu sana ukilinganisha na umri wake aliodeclare! Kuna walakini hapa! huyu sio kijana kama inavyosemwa!
Shule ya makunda ipo kata ya kyengege, tarafa ya kinampanda wilaya ya iramba. ukitafuta kwa google map kyengege imeandikwa kengege, ni kama 60km kutoka singida mjini ukielekea mwanza. mwenye jina la mwigulu nchemba yupo hai na anafahamika. huwezi badili jina la marehemu babu yako, utampata wapi umuapishe.