Naibu Waziri aliyehonga wananchi nyama ya ng'ombe 500 alipigwa chini na kachero la uchafuzi

Naibu Waziri aliyehonga wananchi nyama ya ng'ombe 500 alipigwa chini na kachero la uchafuzi

Hao ng'ombe 500 ni waturuki hutoa sadaka siku ya Eid Ul-Adha huyo mbunge alijipenyeza tu akajipa ujiko.
 
View attachment 3465449

Hajafanya lolote jimboni.

Siku alipoibuka kaja na ng'ombe 500. Achinje wamchague.

Ng'ombe mmoja kumnunua na kumsafirisha na kumchinja na kumpika na vinywaji na kuandaa tukio kadirio la chini laki 8.

Laki nane X 500 = 400 milioni

Umepata wapi hela hiyo ya kuchoma siku moja, akajibu nimepewa na rafiki zangu wa Kituruki.

Yani umetudharau kiasi gani kutulisha nyama siku moja tukuchague. Umewapa nini Waturuki, mapori yetu ?

Mungu hadhihakiwi bana. Na Mungu sifa yake moja anaweza kumtumia yeyote kubeba ujumbe wake. Kuna haramia moja mikono imejaa damu za Wakristo, linaitwa Mtume Paulo. Mungu alikuja akamuinua, akamtumia.

Safari hii Mungu akalitumia kachero moja nguli la kuratibu chaguzi za CCM. Ndo lilikuwa in charge awamu ya tano.

This time likaingia fronti lenyewe jimboni. Likamghalagaza vibaya mno huyu naibu waziri na mgombea wa hela za Waturuki. Na nyama watu wamekula vile vile.

Mungu halali. Dharau ya nyama Mungu kalipa.
Huyo mbunge alijipendekeza kwenye shughuli isiyomhusu.

Waturuki wanachinja ng'ombe kila sehemu na kugawa misikitini wakati wa sikukuu ya Iddi.
 
Acha ujinga hakukuwa na ulazima wa kuficha si ungemtaja tu kwamba huyo naibu Wazir ni Sagini na aliyempindua ni Mahera Kule Butiama?
'Sam Mahera'- Wa ITV kipindi Cha Kampeni za Hayati Edward Lowassa?
 
Hiyo ni rushwa ndogo ukilinganisha na anayetoa rushwa ya baiskeli,pikipiki,magari Nchi NZIMA(mama kizimkazi)

Milioni 400 mpaka 500 kuichoma siku moja sio rushwa ndogo. Ni kubwa.

Mpaka akaona aseme hela sio yake, maana kusema anayo ni nyingi mno.

Kuna watu wanayo milioni 400 mfuko wa shati wanajengea msichana nyumba ya pembeni. Lakini sio kwa watu wa jimbo lile. Wanawake wote wanauza ndizi soko la Kiabakari. Hakuna hata shamba moja la zao la biashara jimboni. Hakuna mtu anamudu kununua sato mmoja kutoka ziwani. Hawafugi, ving'ombe vimechoka mbaya, tembea jimboni ulizia unataka kununua lita tano za maziwa fresh. Good luck circling around.

Kwenye mitera yao ( ndio masoko) hakuna hata mchicha, hata dagaa hakuna. Kuna mihogo michanga na vi chinese vimetoboka toboka vibayaaa!

Shule, ni zile za Lowassa. Wanafeli kama wote. Fredrick Lowassa anasema legacy ya babaake ni shule zile. Wewe Freddy mtoto wako ulimpeleka shule za babaako? Sasa mlimjengea mtoto wa nani asome wakora nyinyi ??? Bora na ye kapigwa chini na li ngwini lenzake la CCM. Mbwa kala mbwa.

Naibu Waziri anaona hawa watu ni mbwa, dawa yao fupa la nyama. Bora na yeye kaliwa kichwa na kachero la Magufuli.
 
Back
Top Bottom