Naibu Waziri atangaza Siku 14 kuondoa namba za 3D, madereva wa serikali kukiona

Naibu Waziri atangaza Siku 14 kuondoa namba za 3D, madereva wa serikali kukiona

Hapo tatizo sio namba za 3D bali ni yule jamaa anaetengeza hizo namba akishilikiana na TBS ili asiendee kulala njaa. Watu ni wanjanja sana nchi hii ....Masasi, Kiboko & Co wameona isiwe kesi wameamua kukimbilia polisi na wao wale hata 10%, kwa tamko hili madereva mjipange na hela za chenchi za buku buku zakuwapoza la sivyo huko barabarani patawaka moto si kichaa kapewa rungu
Mkuu hata hawawezi lala njaa, maana ukinunua gari lazima atengeneze yeye kwanza kisha wewe ndipo uje ubandike 3d juu yake.
So, huendi moja kwa moja ukajitengenezea kibati na kujibandikia 3d, 3d inabandikwa juu ya kibati ambacho tayari huyo jamaa ashaprint namba za kawaida.
 
Kila nikisikia hii marufuku sioni wakifanya rejea ya kifungu gani hasa kimevunjwa? Wanatoa tuu kauli za jumla kwamba wamekiuka sheria. Hivi akitokea mtu akafungua kesi kuitaka mahakama iwatake walete ushahidi wa kifungu mahususi kilichovunjwa watamuona mbaya??
ingekuwa taifa la marekan ningeenda kushitaki ila kwa tz unaweza jikuta unafungwa mfungua kesi mahakama zipo mfukon mwa viongozi
 
Hivi vituko vipo Tanzania tu, huwezi vikuta sehemu yeyote ya ulimwenguni. Raia tubadilike mindset zetu aisee. Mtu anaridhika kufanyiwa upumbavu na serikali maisha yote ila ukimgusa mkewe tu yupo radhi aende jela yani lazma afanye reaction mbaya tu.

Hatuna uchungu na maisha yetu kabisa, wao wafanye wanavyotaka tu kila kitu chema tunafanyiwa kama hisani. We seem to be the most Stupid Citizens on earth.

Wao wakikosea hawaguswi, raia akienda kinyume ni mlolongo wa vitisho na kelele za mujibu wa sheria. Double standards kwanini?
Kumbe huwa unakasirikaga.

Unatisha
 
Kuna taa zinawekwa kwenye magari zinamwanga mkali sana zikikupiga huoni mbele vizuri kwa magari na pikipiki.Naomba askari usiku wafanye zoezi la kukamata magari haya ma pikipiki zenye mwanga mkali ambazo si original kwenye matumizi ya magari na pia maduka wanayouza hizo taa wakamatwe hao wanaouza.Mi najua serikali ina mkono mrefu
 
Hapo utakuta MASASI SIGN katoa mpunga mrefu zoezi lifanyike ili yeye apige pesa.

Namshangaa Waziri anaongelea stika anaacha NGAO zilizopo kwenye Bajaj na Daladala
Na alivyo na uwezo mdogo ameenda straight bila kujiongeza.....huyu masasi kwa miaka mingi amepiga hela ula tamaa na wivu baada ya kuona soko lipo wazi na wengine wanapata kaumia.
Wasichokijua hata huyo sagini dunia imebadilika sana....it's too late...
 
Kuna taa zinawekwa kwenye magari zinamwanga mkali sana zikikupiga huoni mbele vizuri kwa magari na pikipiki.Naomba askari usiku wafanye zoezi la kukamata magari haya ma pikipiki zenye mwanga mkali ambazo si original kwenye matumizi ya magari na pia maduka wanayouza hizo taa wakamatwe hao wanaouza.Mi najua serikali ina mkono mrefu
Exactly ila wenye maduka hawana kosa kwani wanalipa kodi na stahiki zote..
Sorry to say viongozi wengi wana IQ ndogo sana.
Tunga sheria then mtu akikiuka hatua stahiki zichuliwe Period.
Haya matamko ya hewani yabaki katika level ya familia binafsi.
Nchi haiongozi hivi ..haya mi matokeo ya corruption.
Hata JPM kuna mambo alichemka kwa sababu hakuna sheria iliyomuongoza.
Swali dogo tu kwa nini namba atengeze MASASI peke yake kwenye dunia ya sasa?....
Time will tell
 
Aliyesema Tanzania ni channel ya vichekesho huko mbinguni hakukosea

Nchi kama nchi ina mambo mengi ya kujadili maslahi ya wananchi kama umeme, maji, shule, miundombinu, NHIF afya, bei za vyakula n.k

Lakini mkazo unatiliwa kwenye very minor ishu ambayo haina mashiko kisheria.. Damn!

Kuna mchangiaji hapo juu kasema huu ni mradi wa mtu wapige 10% na wazalishaji sasa naanza kuelewa....

Camera zenyewe wanazosema za kusomea hizo plate number ni very local...wenzetu ulaya wameshavuka huko hawana mambo ya kuanza kukimbizana na tuvitu vidogo

Yaani hii nchi kuna muda inakera basi tu
 
Nafikiri tatizo sio namba tatizo ni maslahi.
Sioni ubaya kuwa na namba za 3D ila ungewekwa utaratibu wa kuziboresha zionekane hata zaidi ya mita 100.Pili tamko la waziri halina vifungu vya sheria vya kuzuia namba hizo.
Tatu, serikali iangalie biashara huria ili mradi utaratibu ufuatwe.Mtu achague bidhaa tofauti sokoni ili kumridhisha mteja kuliko kuzuia uhuru wa mlaji.
Sahihi
 
Hivi vituko vipo Tanzania tu, huwezi vikuta sehemu yeyote ya ulimwenguni. Raia tubadilike mindset zetu aisee. Mtu anaridhika kufanyiwa upumbavu na serikali maisha yote ila ukimgusa mkewe tu yupo radhi aende jela yani lazma afanye reaction mbaya tu.

Hatuna uchungu na maisha yetu kabisa, wao wafanye wanavyotaka tu kila kitu chema tunafanyiwa kama hisani. We seem to be the most Stupid Citizens on earth.

Wao wakikosea hawaguswi, raia akienda kinyume ni mlolongo wa vitisho na kelele za mujibu wa sheria. Double standards kwanini?
Nakubaliana na wewe kwa asilimia zote
 
Hapo tatizo sio namba za 3D bali ni yule jamaa anaetengeza hizo namba akishilikiana na TBS ili asiendee kulala njaa. Watu ni wanjanja sana nchi hii ....Masasi, Kiboko & Co wameona isiwe kesi wameamua kukimbilia polisi na wao wale hata 10%, kwa tamko hili madereva mjipange na hela za chenchi za buku buku zakuwapoza la sivyo huko barabarani patawaka moto si kichaa kapewa rungu
wanaotengeneza Plate number za 3D wenyew hawatengenezi hivyo visahani vinavyokuja na hizo namba, bali wao huongeza namba za 3D juu ya namba zilizo kwenye visahani✍️🧠 Nadhani kuna sababu wanazojua wao, ingawa hata zakwao hazina mashiko sana, Sisi nchi yetu inangojea ugundue kitu ikukataze kwakusem hufuat sheria, Lakin hawana mawazo ya kuwaunga mkono walio gundua jambo fulani, hao ni vijana wanatafut kula, ajira umewanyima, wamekuw wabunifu bdo vikwazo kibao, uongoz wetu unahitaji kujichunguza
 
Japo sina ndinga binafsi sizipendi kichizi
 
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetangaza siku 14 kwa watumiaji wa Vyombo vya Moto barabarani kuondoa namba za magari zilizoongezwa ukubwa maarufu kama (3D) na Vimulimuli kwa magari yote yasiyoruhusiwa kuwekwa, namba zote zenye vibao vyeusi na zizonatumia namba za chasis, taa zozote na stika ambazo zimeongezwa kwa matakwa ya wamiliki au madereva.
View attachment 2924898
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini
Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya Kikao cha Baraza la Taifa la Usalama Barabarani leo Machi 04, 2024 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Mhe. Jumanne Sagini (Mb) alisema kuwa namba hizo hazitengenezwi na wakala aliyepata kibali kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS), bali zinatengenezwa kiholela mtaani na herufi hizo kubandikwa juu ya namba halali na kutosomeka katika umbali unaotakiwa ambapo katika viwango vya TBS namba ya chombo cha moto isomeke kwa umbali usiopunga mita 100 ambapo 3D haifiki kiwango hicho.

"Mambo yote yanayohusiana na Usalama Barabarani hufanywa kwa mujibu wa sheria sio utashi wa mtu mmoja mmoja au binafsi kwa mujibu wa usalama barabarani kuhusu matumizi ya namba yamebainishwa vizuri sana na sheria kwamba Namba zinazowekwa zinatakiwa ziweje? ziwe zimeandikwa na nani? anayetambulika na nani? ziwe na ubora gani? namba hizi zote hazijawekwa kwa bahati mbaya," Alisema Sagini
Mhe. Sagini alisema kuwa, Ving'ora vinatoa ishara fulani ili magari mengine yaweza kupisha na hapa nisisitize kuwa, magari yanayotakiwa kuwekwa Ving'ora yanajulikana kama ya Polisi, Zimamoto ya Wagonjwa na yale yaliyopo katika misafara ya Viongozi kufanya hivyo bila kibali maalum ni ukiukwaji wa sheria.

Aidha, Naibu Waziri Sagini alisema kuwa, zoezi la ubanduaji wa namba zilizoongezwa ukubwa litaendeshwa hata kwenye magari ya Serikali ambapo yakibainika na makosa ya namna hiyo wanaotumia watachukuliwa hatua.

Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Polisi DCP Ramadhani Ng'anzi alisema kuwa, wanapiga marufuku namba zilizoongezeka ukubwa kwa sababu kiusalama Namba za 3D sio salama na namba za magari lazima ziwe 2D kutokana na mifumo na kamera kutotambua 3D.

"Baada ya Tarehe 15 Machi, 2024 tutaendelea kuzibandua na tukiona ile plate namba haisomeki vizuri tutakukamata na hili zoezi mnatakiwa muondoe wenyewe kwa hiyari lasivyo Jeshi la Polisi litakukamata kwa kuvunja sheria hata tukikuta namba haisomeki vizuri yaani imechubuka," Alisema.

Aidha, Kamanda Ng'anzi aliongezea kuwa, Operesheni itajumuisha na Taa/Sport light kinyume na taratibu za mtengenezaji au kibali kutoka kwa Mkaguzi wa magari na uwekaji wa stika za rangi mbalimbali kwenye taa kubwa mbele na nyuma ya gari, ambazo zinabadilisha mwanga wa taa halisi mfano stika nyeusi, blue nyekundu na tinted.
Hizo 3D hazina ubora wala uzuri wowote
 
Back
Top Bottom