PreGE2025 Naibu Waziri Deus Sangu: Mimi ni mafia, nitawashughulikia wanaotaka kugombea jimbo la Kwela

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Your browser is not able to display this video.

Mbunge wa Jimbo la Kwela, Deus Sangu, ametangaza hadharani kuwa yuko tayari kutumia mbinu kali kushughulikia watakaothubutu kugombea ubunge katika jimbo hilo. Aidha, ametishia kuwashambulia na kuwaumiza watu wanaochapisha taarifa kumhusu kwenye mitandao ya kijamii.

Katika kauli zake, Sangu amedai kuwa yeye ni jasusi aliyefunzwa na serikali kupitia Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), akisisitiza kuwa mafunzo hayo anayatumia kuwazuia watu asiowataka kuingia au kushindana naye kisiasa ndani ya jimbo la Kwela.

Amedai kuwa kwa kutumia mbinu hizo, amefanikisha kulizuia jimbo hilo kugawanywa kinyume na mipango ya serikali na chama tawala (CCM), akisisitiza kuwa yeye pekee ana uwezo wa kulilinda jimbo hilo kubaki chini ya ushawishi wake kwa njia yoyote itakayohitajika.

Kauli hizo zimeibua taharuki miongoni mwa wananchi na wadau wa demokrasia, huku baadhi wakidai kuwa ni hatari kwa usalama na uhuru wa kisiasa katika eneo hilo.
 
Vipi wana CCM wenzake watakaolitaka hilo jimbo??
 
Nchi zilizo staarabika huyu angeshavuliwa ubunge, hii ndio uhaini wenyewe.

Na speaker yupi tu anatoa macho?
 
Kwa muda wa miaka 5 tu atakuwa ametengeneza zaidi ya bilioni 10, lakini kuna mtumishi wa umma amefanya kazi miaka 40 hajatengeneza hata milioni 200. Ni ujinga ujinga tu
 
Huyu ni wa kufungwa, ni marufuku mwana usalama ku expose his past ama identity yake.
Huyu ni mjinga kama wajinga wengine
Si ajabu hajawahi serve kokote pumbav zake

Lakin kauli za kusema atapoteza watu anatakiwa achukuliwe hatua za kinidham, ni kosa kisheria na ni upumbavu wa hali ya juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…