Naibu Waziri Dugange Aipongeza TARURA kwa Kazi Nzuri ya Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara

Naibu Waziri Dugange Aipongeza TARURA kwa Kazi Nzuri ya Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

Naibu Waziri Dugange aipongeza TARURA kwa kazi nzuri ya Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. Festo Dugange ameipongeza TARURA kwa kazi nzuri ya ujenzi wa miundombinu ya barabara nchini.

Pongezi hizo amezitoa wakati alipotembelea mabanda ambayo yapo chini ya TAMISEMI katika maonesho ya Nanenane yaliyofanyika kitaifa Mkoani Mbeya.

"Kimsingi niwapongeze mnafanya kazi nzuri kuhakikisha kwamba barabara zetu za mijini na vijijini zinapitika vizuri zaidi" alisema Mhe. Dugange.

Akizungumzia ongezeko la bajeti ya TARURA, Mhe. Dugange alisema kuwa ndani ya miaka miwili na nusu, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza bajeti ya Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kutoka shilingi bilioni 250 mpaka shilingi trilioni 1.2 ambayo ni zaidi ya mara nne ya bajeti.

Kwa upande mwingine Mhe. Dugange alikiri kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanya kutokana na ukweli kuwa nchi yetu ni kubwa na mtandao wa barabara unaohudumiwa na TARURA ni Mkubwa sana.

Mhe. Dugange alitumia fursa hiyo kutoa wito Kwa TARURA kuendelea kuweka mipango ya kuhakikisha kwamba wanatumia teknolojia mbadala ya ujenzi wa barabara na kuongeza wigo wa kutumia teknolojia hiyo ambayo kimsingi anaamini miundombinu ya barabara itadumu kwa muda mrefu zaidi.

Pia, Mhe. Naibu Waziri amewataka TARURA waendelee kuhakikisha kuwa miundombinu ya barabara inajengwa kwa ubora Kwa kuzingatia thamani ya fedha lakini inakamilika kwa wakati.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-08-14 at 13.43.37.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-14 at 13.43.37.jpeg
    36.4 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-08-14 at 13.47.08.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-14 at 13.47.08.jpeg
    38.1 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-08-14 at 13.48.57.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-14 at 13.48.57.jpeg
    41.4 KB · Views: 4
Back
Top Bottom