change formula
JF-Expert Member
- Sep 8, 2020
- 729
- 1,559
Tangu huyu ndugu anayeitwa Hamis Mwinjuma ,maarufu Mwana FA ateuliwe na Rais kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Michezo ameonesha kuwa hatoshi kuwa kwenye nafasi hiyo.
Ni mtu hatari kwa usalama na ustawi wa amani na utulivu wa nchi.
Tangu ateuliwe nafasi hiyo amekuwa anatumia muda mwingi kwenye ofisi za wafadhili wake pale posta kwenye jengo la Suremander tower kwa mfanyabiashara maarufu anaejulikana kama GSM.
Amekuwa anatumia ukaribu wake na mfanyabiashara huyo kwa kutumia nafasi yake ya Unaibu Waziri kutekeleza matakwa ya mfanyabiashara huyo bila kujali kuwa ni hatari kwa afya ya ustawi wa sekta anayoisimamia kama Naibu Waziri.
Sote tunajua GSM anamiliki na kufadhili baadhi ya vilabu vya michezo hasa mpira wa miguu, hivyo kitendo cha Naibu Waziri kugeuza ofisi za mfanyabiashara huyo kama nyumbani kwake, kunatishia uhai wa sekta ya michezo na hii inaweza kuleta sintofahamu na kutishia amani na ustawi na ustaarabu wa nchi yetu uliojengwa kwa miaka mingi.
Tangu Hamis Mwinjuma, apate nafasi hii ya Unaibu Waziri, timu inayomilikiwa kinyemela na GSM, Young African (Yanga) imekuwa ikipata upendeleo wa shahili dhahili kutoka Serikalini na hii inaleta sintofahamu kwa washabiki wa vilabu vingine vya michezo hasa Simba SC ambayo mashabiki wake wamevumilia hali hio kwa muda mrefu na sasa wameanza kutoka hadharani kulalamika
Hii ni hatari!! huu upendeleo kwa timu ya Yanga ni juhudi za Naibu Waziri huyo kumfurahisha GSM kwa manufaa yake.
Serikali isipokuwa macho na kuchukua hatua kwa Naibu Waziri huyu mwenye mahaba mazito na mfanyabiashara uyo (GSM) inawezekana ikaleta hatari kwa ustawi wa nchi yetu.
Mashabiki wa Simba wanaweza kuingia barabarani kuandamana kupinga upendeleo wa wazi wazi unaofanywa na Serikali kupitia Naibu Waziri huyo.
Kama Serikali inaona Yanga ndio Klabu pekee hapa nchini basi itangaze rasmi Watanzania wote wajue na sio kufanya upendeleo usio na afya kwa taifa letu. Wote tunajua taifa letu limegawanyika pande mbili za Simba na Yanga kwenye suala la michezo!
Haiwezekani Simba ambayo kwa miaka zaidi ya mitano inawakilisha taifa kwa mafanikio makubwa haijawahi kupewa sapoti yoyote na Serikali. Ila Yanga ambayo imekuwa ikitia aibu taifa inapata misaada ya wazi na ya kificho kutoka serikalini kwa msaada wa Naibu Waziri huyo kwa manufaa anayojua yeye.
Naibu Waziri kushinda kwenye ofisi za mfanyabiashara ni hatari! Inawezekana kuna biashara haramu inafanyika hapo maana si jambo la kawaida! Huyo Naibu Waziri ikitokea akawa Waziri kamili (MUNGU aepushie mbali) siri zote za vikao vya baraza la mawaziri zitakuwa wazi.
Vijana wanaopata nafasi hizi za uongozi ni vyema kuzingatia maadili, waache tamaa za kutaka utajiri haramu wa haraka!
Kuna mengi sana mambo haramu juu ya Naibu Waziri huyu hafai kabisa na Rais amtoe kwenye nafasi hiyo.