Naibu Waziri Hamis Mwinjuma 'Mwana FA' ni kirusi kwa ustawi wa michezo, Rais amtoe wizarani

Hilo liko wazi kuna upendeleo, uswahiba wa fa na salah ni mkubwa sana.

Mie ni shabiki kindakindaki wa simba lakini katu siwezi ingia barabarani kisa yanga kapendelewa,😂 uchizi huo sina.

Nimeshindwa kuingia barabarani kwa vitu vya msingi vya taifa ambavyo vinanikera na kunisokota rohoni, wizi wa wazi wazi wa viongozi, mara bima,mara mafao ya wenza, mara hiki mara kile, siwezi ingi road kisa simba
 
Hivyo unaona ni sifa kwa kiongozi wa umma kuwa karibu sana na wafanya biashara wenye historia ya ukwepaji kodi? Watanzania tuache ujinga tukemee viongozi wa siasa wanaotaka kushinda kwenye ofisi za wafanyabiashara
Kama Rais yupo karibu na wafanyabiashara unaona ajabu naibu waziri tena wa michezo kuwa karibu na wafanyabiashara?

By the way kwani ww unatatizo gani na wafanyabiashara? Si ndio wanaoongoza kulipa kodi Tz na kila siku mapato yanapaa kwa kodi zao.

Kama Huna hoja kakojoe ulale kolo.
 
Ndivyo alivyosema hivyo?
 
Watanzania wengi ni wachoyo, wabinafsi, wasiopenda maendeleo ya wengine (ingawa wao hawafanyi juhudi zozote za maaña kùjikwamua zaidi ya kuuza karanga kwa kijiko), wenye kupenda kuharibiana ugali, wasio na matumaini, sifa nyingine malizieni
Wanatumia vyeo vyao kujinufaisha wao na marafiki zao! Mfano ilo fungu la kusafirisha mashabiki limetoka kwenye hesabu ipi? Unasafirisha mashabiki unawapa malazi,chakula n.k wakati hapo muhimbili watu wanakufa kwa kukosa Panadol! Ekueme!!
 
Mimi naona umeandika kichuki zaidi. Yanga imependelewa kipi? Na F.A hawezi kuua urafiki na GSM kwa sababu ya uwaziri kumbuka kuna wakati alimfaa na kuna kurudi mtaani. Lazima awe na hatua ya kuanzia jinsi ya kuishi mtaani. GSM ni nguli wa biashara. Unajuaje kama anatafuta fursa za kujifunza jinsi ya kuendesha biashara na connection zake kabla hajatoka kwenye madaraka pindi ambayo huenda asiwe na access ya kukutana na GSM?
 
Kwa hiyo Simba mnataka Serikali iwasaidie kwenye usajili?

Acheni kelele nyie kaeni chini na huyo Yung Milionea wenu mumuombe atoe pesa ili msajili wachezaji wazuri na sio hizi blabla.

Alafu hao mashabiki wa Simba eti Milioni 30 ni kina nani? au ulikuwa unazungumzia fedha za Mo?
 
Nini kikubwa kinahusu ukaribu wao? Tujuze em

Salah alikuwa anapenda tu mziki wa hip pop. Mziki ndio sababu kuu ya ukaribu wao. Pia salah alikuwa mambo safi kitambo hivyo wasanii walimpenda sababu anawapa vihela wakiwa na shida
 
Mabadiliko uanza na chochote! Unajua maandamano yalioanzia Tunisia yakasambaa arabuni kote maarufu kama maandamano ya asumini yalitokana na nini? Usidharau chunusi inaweza kuleta jipu.
 
Wakati Simba inapewa ndege na serikali ulikuwa bado upo Kijijini?
 
Kwani mlezi wenu kipenzi Wallace Karia na Bodi yake ya ligi anasemaje?

Dr. Damas Ndumbaro, mwanasheria na wakili wenu wa zamani naye anasemaje? PM na Spika nao wana hizi taarifa za wewe shabiki kulia lia humu jukwaani, huku ukiwa huna ushahidi wowote ule wa hizo shutuma zako?
 
Nakumbuka biashala United ilishindwa kusafili inamana hili fungu kipindi Hiko halikiwepo
Kuna watu ni wapuuzi Sana humu, tumeandika humu mara nyingi tu, Simba na Yanga ni timu zinazomilikiwa na serikali sijui lini mtaelewa Kiswahili.

Muulizeni Mo Kwa nini anakwama kuimiliki Simba?

Yani wewe unataka kuipangia serikali juu ya timu zake?
 
Hao wafanyabiashara waliwahi kujibu tetesi zao za ukwepaji kodi enzi za awamu ya nne?! Tafakali chukua hatua hata kimoyo moyo!
 
Sasa mwana fa asiongee na watu wewe ndo ufurahi
Kwani uwaziri ni jela hapaswi kuongea na watu

Simba hawakuomba
Wenzao yanga wakaomba na aombaye hupewa kwaiyo Waziri angetoa msaada kwa watu wasiohitaji

Badala ulaumu viongozi wa mbumbumbu wasiojiongeza wewe unamlaumu Waziri

Ndo maana tutamheshimu Rage aliyewapa jina la mbumbumbu
 
Kuna watu ni wapuuzi Sana humu, tumeandika humu mara nyingi tu, Simba na Yanga ni timu zinazomilikiwa na serikali sijui lini mtaelewa Kiswahili.

Muulizeni Mo Kwa nini anakwama kuimiliki Simba?

Yani wewe unataka kuipangia serikali juu ya timu zake?
Kwa hiyo Nani mpuuzi sasa ndugu Mimi au wewe ambaye unajifanya kujua Sana imana selkali kama mzazi anabagua watoto wake
 
Unajua sheria za maadili ya viongozi wa utumishi wa umma!! Au unaenda kipunda punda tu! Uku nilipo mwanasiasa kuwa karibu na mfanyabiashara kupitiliza lazima ufanyike uchunguzi! Bongo uchawa mwingi ndio maana mpaka leo hadi vyoo tu mashuleni kujenga mpaka msaada wa US aid.
 
Kwa jili ya maslahi ya taifa, nitakuwa radhi kuadamana lakini sio huu upuuzi wa simba tunaonewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…