Naibu Waziri Hamis Mwinjuma 'Mwana FA' ni kirusi kwa ustawi wa michezo, Rais amtoe wizarani

Sio kwamba wewe ndio kapuku ndugu kapuku? Chotus Chama analamba milioni 40 kwa mwezi, haya wewe kapuku endelea kukaa hapo hapo kwa shem, utaisoma namba mamamaeh.
Mngekua na utajiri msingelilia msaada kutoka serekalini
 
MwanaFA ni Simba damu
WanaTA ni Simba damu
 
Oooh wametoka mbali...Oooh hamjui walikotoka!..Mbali wapi?...Au walikuwa wanananihii?
 
Wivu unakusumbua sana.
 
Kuna waziri wa Michezo simba damu,kuna waziri mkuu nae ni simba damu..rais wa tff ni simba damu..hawa wote wameshindwa kuisaidia Simba mpk lawama upeleke kwa mtu mmoja tu ambae nae ni Simba damu au una chuki zako binafs mkuu..au wivu unakusumbua???
Ukisikia "BAT ma" ndio huyo.
 
Ndumbalo sasa hivi sisimkii.. naona kaamua kukaa pembeni
 
Mwana FA na akina GSM washikaji tangu hata hajawa mbunge na Farouk Baghoza. So, kuwa waziri haimaanishi ushikaji utaisha.
 
Tokea namba moja alivyoenda na Yanga kwenye ile safari yao kuzindua jrzi Ikulu ya Malawi machawa wote walijitokeza na kujipendekeza kila linapotokea jambo la Yanga..

Rais ameinyesha mapenzi ya wazi na wasaidizi wake wameunga tela.
 
being fair performance na change zinazotokea kwenye klabu ya Young African ni matokeo ya moja kwa moja ya uongozi bora na mikakati inapangwa na kutekelezwa huwezi sema simba inahujumiwa na Deputy ngali muda huo simba sc na uongozi wake wapo kama hawapo
 
Jana nilimsikia akisema wenzetu nao wameleta maimbi ili serikali iwape msaada. Kuna kipande akasema "kama tulivyoongea pale jangwani tulipokuwa tunawaaga waliotangulia na bus". Binafsi nikaona kumbe Waziri wa michezo kujionyesha hadharani kuwa yu upande fulani sio kosa kwa mujibu wa serikali ya mama saa 100?
Huyu ndie bongo fleva anaetia aibu ukimlinganisha na wengine waliomtangulia bungeni. Sawa tinajua Yanga ni timu ya ccm hatukatai ila ukishakuwa waziri unatakiwa kujua hauongozi wana Yanga au wana ccm peke yao, tunamuona Mwigulu, ni yanga lialia ila hawezi kujianika hadharani kwasababu ya ukomavu wa akili.
Saa 100 sijui aliona nini kwa huyu bongo flavor, sijui alishawishika na nini!!.
 
Huenda unajua au unajifanya hujui
Lakini naomba nkukumbushe hao unao lalamika kuwa naibu waziri anashinda ofisini kwao hao ndio wenye mchango mkubwa 80% kumfanya huyo bwana kuwa hapo na kumwita mbunge na hata naibu waziri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…