Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHE. KATIMBA - KAMILISHENI MIRADI KWA WAKATI KUHARAKISHA TIJA KWA WANANCHI
Naibu Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba (Mb) amemtaka Mkandarasi na Mtaalamu Mshauri anayetekeleza Mkataba wa Ujenzi wa miundombinu inayoratibiwa na mradi wa TACTIC wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kukamilisha haraka ujenzi huo kulingana na matakwa ya mkataba ili wananchi wanufaike kikamilifu na uwekezaji huo unaosimamiwa na Serikali kupitia TAMISEMI.
Naibu Waziri Katimba amesema hayo leo Disemba 04, 2024 Mjini Kahama, Shinyanga, wakati wa utiaji saini mkataba wa Ujenzi wa Kituo Kikuu cha mabasi eneo la Mbulu, Ujenzi wa Soko la Sango pamoja na ujenzi wa kituo kidogo cha Mabasi na Soko la Wajasiriamali wadogo eneo la Zongomera Wilayani Kahama, akisema kukamilika kwa miradi hiyo kunaenda kukuza na kuimarisha uchumi wa mwananchi na kukuza pato la Mkoa wa Shinyanga.
Mhe. Katimba ametoa kauli hiyo mara baada ya kupata malalamiko kadhaa kutoka kwa Viongozi mbalimbali mkoani Shinyanga, wakilalamikia mwendo usioridhisha wa Mkandarasi M/S Sichuan Road and Bridge (Group) Corporation Ltd anayetekeleza ujenzi wa barabara za Mjini, Barabara ya kuingia kituo cha Wajasiriamali cha Zongomela pamoja na mitaro ya kutiririsha maji ya Mvua kwenye Halamshauri ya Mji wa Kahama.
Kufuatia maelekezo hayo, Mhe. Katimba ametembelea na kukagua miradi hiyo inayolalamikiwa na kupata maoni ya wadau mbalimbali, akiahidi Kumshauri Waziri wa nchi- TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa(Mb) kuhusu hatua za kuchukua kwa Mkandarasi huyo anayesuasa katika utekelezaji wa mradi huo kwa kwenda kinyume na Mkataba na hivyo kusababisha kuchelewa kwa tija ya uwekezaji huo.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Katimba amemuagiza Mtaalamu mshauri na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kahama kuhakikisha kuwa mikataba inasimamiwa vizuri ili kuwezesha kukamilika ndani ya muda uliopangwa, kwa ubora tarajiwa huku thamani ya fedha iliyotumika ikitakiwa kuonekana kwa ukamilifu wake.
Aidha Mhe. Katimba alisema uboreshaji wa miundombinu ya barabara unaofanywa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia TARURA, umepelekea ongezeko kubwa la bajeti ya TARURA kutoka Bilioni 275 hadi Bilioni 710 kwa mwaka
Attachments
-
Gd-UJVtWMAAkvhS.jpg103.9 KB · Views: 4 -
Gd-UJVvXMAAnApa.jpg127.9 KB · Views: 4 -
Gd-UJVuXYAAnqW0.jpg144.9 KB · Views: 6 -
Gd9HxLEXMAA_lwF.jpg446.9 KB · Views: 6 -
Gd9HxLBXAAAmt0_.jpg490.4 KB · Views: 4 -
Gd9HxLAWIAAQQ0H.jpg330.9 KB · Views: 4 -
Gd8pDqjXMAAjYen.jpg261.8 KB · Views: 4 -
Gd8pDppXAAA4pEk.jpg295.8 KB · Views: 4 -
Gd8pDrCWkAAQDbU.jpg338.8 KB · Views: 4 -
Gd9vWQaWMAAkmGD.jpg383.2 KB · Views: 5 -
Gd9vWQaW8AA3rcr.jpg501.1 KB · Views: 5