Naibu Waziri Kihenzile: Miradi itekelezwe kwa kuzingatia Muda na Thamani ya Fedha

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

NAIBU WAZIRI KIHENZILE: MIRADI ITEKELEZWE KWA KUZINGATIA MUDA NA THAMANI YA FEDHA


"Nawapongeza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kwa kuweka taa katika uwanja wa ndege wa Dodoma, uwanja huu kwa ripoti kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) inaonesha unashika nafasi ya 4 kwa kuhudumia abiria wengi, nina imani maboresho yakifanyika utapanda zaidi kutoka nafasi hiyo na sababu kubwa ni kwamba Dodoma kuna idadi kubwa ya watu hivi sasa" - Mhe. David Kihenzile, Naibu Waziri wa Uchukuzi.


"Miradi yote inayotekelezwa katika Wizara ya Uchukuzi sharti mojawapo ni kwamba ni lazima izingatie muda. Kama mradi unapaswa kukamilika ndani ya miezi 6 hakikisheni unakamilika ndani ya miezi 6. Serikali haiko tayari kuvumilia uzembe, sababu wala visingizio lakini pia miradi hiyo izingatie thamani ya fedha" - Mhe. David Kihenzile, Naibu Waziri wa Uchukuzi.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…