Naibu Waziri: Mahitaji ya Maji Dodoma ni Lita Milioni 149, uzalishaji ni Lita Milioni 79

Naibu Waziri: Mahitaji ya Maji Dodoma ni Lita Milioni 149, uzalishaji ni Lita Milioni 79

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Naibu Waziri wa Wizaya ya Maji, Mhandisi Kundo Mathew amesema moja ya changamoto ya uhaba wa maji iliyopo Jijini Dodoma ni kuwa uhitaji wa huduma hiyo ni Lita Milioni 149 kwa siku wakati uzalishaji ni Lita Milioni 79 sawa na Asilimia 52.

Amesema Serikali ina mpango wa kuongeza visima maeneo tofauti ya Jiji hilo ili kupunguza ukali wa mgao wa maji.

Pia soma:
~
Kero ya maji safi jijini Dodoma, Waziri Aweso ingilia kati
~ Dodoma: Kazi ya uchimbaji wa kisima eneo la Kisasa utaanza siku ya Jumatatu Oktoba 07, 2024
 
waziri aweso hakustahili kua waziri wa maji ni vile anatoka kanda yenye mtaji wakutosha wa ccm

hana cha maana anachofanya tangu ateuliwe
 
Huyu waziri huwa nahisi anapewa sifa zinazozidi uwezo wake
 
Na huo ndio ukweli. Walitudanganya mwaka 2022 kwamba mwaka jana ndo tatizo la maji Dodoma lingebaki kuwa historia. Tukaletewa miradi mingi ya uchimbaji wa visima kulizunguka Jiji, mapicha kibao ya mabomba ya bluu, picha za magari ya kuchimba visima na nk. Mwaka ukaisha na mateso yakaendelea. Kwa sasa hali ni mbaya kupita maelezo. Kuna sehemu utafikiri watu wanaishi jangwani. Watuambie ukweli tu, kwani ukweli utawaweka huru.
 
Back
Top Bottom