Na huo ndio ukweli. Walitudanganya mwaka 2022 kwamba mwaka jana ndo tatizo la maji Dodoma lingebaki kuwa historia. Tukaletewa miradi mingi ya uchimbaji wa visima kulizunguka Jiji, mapicha kibao ya mabomba ya bluu, picha za magari ya kuchimba visima na nk. Mwaka ukaisha na mateso yakaendelea. Kwa sasa hali ni mbaya kupita maelezo. Kuna sehemu utafikiri watu wanaishi jangwani. Watuambie ukweli tu, kwani ukweli utawaweka huru.