SI KWELI Naibu Waziri Mkuu amewekwa ili kuzuia kuvunjwa Baraza la Mawaziri

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Cheo cha naibu wazuri mkuu hakipo kikatiba ndio maana marehemu Mrema alishindwa kupata mafao ya naibu wazuri mkuu kwa sababu hakikuwepo kwenye muundo was utumishi.
Vyeo hivi Mara nyingi vinakuwepo pale rais anatokea visiwani.
Kwahiyo hapa kwetu rais kavunja katiba na badala yake amefanya hili kwa utashi wake tu.
 
Cheo cha naibu wazuri mkuu hakipo kikatiba ndio maana marehemu Mrema alishindwa kupata mafao ya naibu wazuri mkuu kwa sababu hakikuwepo kwenye muundo was utumishi.
Vyeo hivi Mara nyingi vinakuwepo pale rais anatokea visiwani.
Naomba kuelewa uliposema vyei hivi hutokea kwa Rais anopotokea visiwani
 
Naibu Waziri Mkuu ni cheo alichokileta Rais, hakitambuliki ki-katiba. kwa hiyo endapo Waziri Mkuu akiamua kuachia ngazi basi ni lazima mchakato kama ule wa EL wakati ule ufuatwe wote.

Kwani wakuu mmenusa kitu? mbona maswali haya.
Nimekuelewa mkuu.
Lakini tukumbushane kwamba Lowasa alistaafu na hakujiuzulu.
Kwahivyo mchakato ulifanyika kwasababu waziro mkuu alistaafu
 
Mzee tuendelee kuwinda senene na kuvuna asali.
👉Hi tafakuri yako, isije sababisha tuka Anza kukimbizana nyumbani🤒
 
Hivi kwani Baraza likivunjwa kuna tatizo gani? Rais si atawarudisha mawaziri walewale.

Ishu ingekuwa kama tungerudia uchaguzi mkuu.
Nisawa hakuna tatizo mkuu, ila hapa nimekuja kujifunza tu ili nipate uelewa kutoka kwenu magwiji
 
Sawa mkuu, basi tutegemee lolote kutokea kabla ya huu mwaka kuisha...😊
Acha ramli za kijinga, mbona mawaziri wana manaibu wao, waziri mkuu kuwa na naibu shida iko wapi. Ujue rais alishauriana na waziri mkuu na makamu wa rais kabla ya kuundwa hiyo nafasi. Mmeambiwa atakuwa anamsaidia waziri mkuu kuratibu shughuli za serikali, kuna nini cha ajabu hapo. Fanya kazi achana mambo usiyoyaelewa
 
Hivi cheo cha Naibu Waziri Mkuu hakipaswi kuwa kimetajwa kikatiba? Swali juu ya swali!
 
Hebubacha kumtusi mzee wangu, una mwita mjinga ili iweje🤔.
👉Halafu afabye kazi ili iweje, wakati duniani tuna pita tu😁 Ushimen
 
Naomba kuelewa uliposema vyei hivi hutokea kwa Rais anopotokea visiwani
Naibu waziri mkuu cheo hiki likianza kutolewa wakati was Mwinyi na kimejirudia wakati was Samia.
Nyerere, Mkapa, Kikwete na Magufuli hakujawahi kuwa na upuuzi huo.
 
Unawezaje kuthibitisha hilo,ya kwamba rais Samia ameshauriana na hao wasaidizi wake?
That's Your perception ,hii nchi ni ngumu sana,wanaoendesha nchi hii ni invisible people's
Unaowaona ni wapokea maelekezo tu
 
Nimekuelewa mkuu.
Lakini tukumbushane kwamba Lowasa alistaafu na hakujiuzulu.
Kwahivyo mchakato ulifanyika kwasababu waziro mkuu alistaafu
Lowassa alistaafu lini? Yeye mwenyewe alitangaza bungeni kwamba ameandika barua ya kujiuzulu kwa rais. Lowassa hajawahi kustaafu kamwe.
 
Litavunjwa tuu na lisipovunjwa basi ni lazima livunjike.. Naibu ni sikio wakati pm ni kichwa
 
Nimekuelewa mkuu.
Lakini tukumbushane kwamba Lowasa alistaafu na hakujiuzulu.
Kwahivyo mchakato ulifanyika kwasababu waziro mkuu alistaafu
... kikatiba issue ni uwaziri mkuu kukoma ambako kunaweza kuwa kwa sababu tofauti - kujiuzulu, kufukuzwa, kushindwa kutekeleza majukumu yake especially kwa ugonjwa, ubunge wake kukoma, kufariki, n.k.
 
Kwa kawaida inafahamika kwamba ikitokea Waziri Mkuu amejiuzulu, na Baraza zima la Mawaziri linavunjwa.

Swali langu ni kwamba, Ikiwa Waziri Mkuu atajiuzulu na wakati huo pakiwa na Naibu Waziri Mkuu, Je Baraza la Mawaziri litavunjwa ama halitovunjwa kwasababu tayari patakuwa na Naibu Waziri Mkuu?
 
Kwani waziri mkuu akijiuzulu na baraza lisipovunjwa itakuaje??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…