Naibu Waziri Mkuu atembelea Mradi wa JNHPP asema ndio suluhisho la upatikanaji umeme wa uhakika Nchini

Naibu Waziri Mkuu atembelea Mradi wa JNHPP asema ndio suluhisho la upatikanaji umeme wa uhakika Nchini

shida wabongo huwa tunapangwa sana, Na huwa wepesi sana kupangika katika hoja za namna hii na ndo maana wakati tunasema ngoja tuone ndo mda ambao watu wanafany mambo yao ya uhakika katika kujinufaisha zaid
 
Tanzania bado hata na bwawa bado umeme ni mdogo kuliko mahitaji yatakayo kuwepo mfano

1. Umeme wa treni haujawnza kutumika
2. Viwanda vipya
3. Ongezeka la maendeleo kama nyumba mpya, umeme vijijini
4. Ongezeko la matumizi kama fridge , air condition ….
5. Umeme kupotea kwa kusafiri

Ukitoa hayo hapo tunahitaji bwawa kama tatuView attachment 2751403
Suluhu imeshapatwa kwa JNHPP
 
Sijawahi kusikia Makamba akisema hayo.
Hata kama huwahi kumsikia akiongea lakini hiyo kauli ilishawahi kutolewa na mkurugenzi wa shirika kwa baraka za J Makamba kama waziri mwenye dhamana husika

Kauli tata za serikali ndizo zinazopunguza imani ya wananchi

Tazama hizi hapa chini
1. Jumatatu, 29 Februari 2016-GHARAMA ZA UMEME KUSHUSHWA BEI: SHIRIKA la Umeme (Tanesco) limewasilisha katika Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) maombi ya kushusha bei ya umeme
2. 29 May 2023-
Ewura kuamua bei ya umeme-Mharage Chande:
1695282359445.png

1695282510952.png

1695282632141.png

Wanasiasa ni watu wenye dhuluma na waovu wakubwa wanadanganya wananchi ili wapate kura zao kisha waanze kunufaika wao bila kujali anayelipa hizo gharama ni mwananchi kwa ununuzi wa bidhaa na huduma mbalimbali
 
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko amelipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa usimamizi makini na hatua kubwa iliyofikiwa kwenye ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ambao mpaka sasa umefikia Asilimia 91.72.

Dkt. Biteko ameyasema hayo Septemba 16, 2023 alipofanya ziara katika mradi huo wa kimkakati na kuongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, imefanya kazi kubwa ya kuusimamia kwa karibu mradi huu.
Amesema "Tunashukuru sana Serikali pamoja na Wizara na TANESCO kwa kuhakikisha ujenzi unaenda kwa kasi licha ya kuwepo kwa changamoto ya upungufu wa umeme unaosababishwa na kupungua kwa kina cha maji kwenye mabwawa ya uzalishaji umeme."

Ameongeza kuwa kwa sasa umuhimu ni Watanzania wapate umeme wa uhakika ambapo suluhisho mojawapo ni kukamilika kwa Mradi wa JNHPP.
Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Julius Nyerere ulianza ujenzi wake Disemba 12, 2018 na unagharimu kiasi cha shilingi Trilioni 6.5 na hadi sasa mkandarasi amekwishalipwa kiasi cha shilingi trilioni 5.6 cha malipo yote.

Ziara hii inakuwa ya kwanza kutembelea mradi huu wa kimkakati wa Julius Nyerere tangu ateuliwe na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.

Chanzo: Neema Mbuja, Rufiji
Naona naye ni Kasuku tu,ni yale yale ya Mwitongo,ni lazima apalilie mapema.Very disgusting.
 
Back
Top Bottom