Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko ni Turufu Kuu ya Rais Samia katika kupata Kura nyingi za Kanda ya Ziwa

anzia mwanza, geita, simiyu, shinyanga, haifikishi majimbo 150? Ongeza mikoa mingine waliko, tabora, kigoma, ruvuma, kagera, mara, katavi, rukwa, mbeya, singida, bado majimbo 150 hayatimii? Tatizo wengi ni ccm na hawana muamko wa siasa za mageuzi
Ila kwenye ballot box Wanahit 15ml so hiyo ni namba nzuri kwa mgombea yeyote wa ikulu...sema chadema ni wajinga kitendo Cha kumsema magufuli kwenye mikutano Yao kinawaondolea credibility.
Ni wazi kwamba Sasa tuko kwenye kipindi Cha siasa za kikanda na ukabila. Chadema wange'base na namba ya hili kabila la kisukuma wangevuna pakubwa. Msukuma ni mwepesi kumzuga maana huku ground Samia hapendwi kabisa.
Trust me kura za 2025 zitaamliwa na polisi na wizi chadema wakikaa vizuri. Ila kwenye sanduku la kura akisimama Samia chadema wanatangazwa saa nne asubuh
 
Huwa nashangaa nikisikia mtu anaamini chama cha majambazi kinafanya kitu ili kipate ushawishi wa wapigakura.

Mazee chama cha majambazi hakitegemei makaratasi, kuingia madarakani. Chama cha majambazi kinategemea tume na polisi.
 
Fact , umeona mbalii
 
Gig president in a gig economy!!
 
Hakika na KILIMANJARO inarudi kuwa ngome ya CHADEMA, kilimanjaro imechukiwa sana na watawala, imetengwa sana lakini haitoshuka.
 
Kiasi, changamoto ni mifugo kuvamia mashamba na rushwa za kuzuia haki.
 
Kanda ya ziwa CHADEMA wazichange karata zao vizuri kuing'oa CCM huko. Wakifanikiwa huko, asubuhi na mapema wanatangazwa washindi
 
Ndio lengo ili kuwahadaa wasukuma,cheo Cha unaibu wzr mkuu ni ubatili kwa sheria ipi
 
Kanda ya ziwa CHADEMA wazichange karata zao vizuri kuing'oa CCM huko. Wakifanikiwa huko, asubuhi na mapema wanatangazwa washindi
Ccm wameliona Hilo ngoja tuone Wasukuma watahadaika
 
Sema mazao anakosea sana kuwaondoa vibarua wa Magufuli shambani kama mmiliki mpya wa shamba kwa kuhofia mazao hayatakomaa.
 
Rais Magufuli wakati yupo hai aliwaimarisha sana Wasukuma na kuwafanya wawe wamoja, sasa baada ya kufa walisambaa sana kama kondoo waliokosa mchungaji.

Sasa kule Kanda ya Ziwa Wasukuma bado wanaamini Magufuri hana mbadala, hawana habari kabisa na Rais Samia. Picha Hayati Magufuri bado zinatamba kwenye hoteli na saloon, wananchi wa kawaida bado hawapo na Rais Samia!

Sasa Rais Samia ametafakari vizuri kuwapelekea Biteko ili awakusanye awarejeshe kwenye ule umoja na kuwafanya waanze kuwa na imani nae na hii ndio kazi kuu ya Biteko, kuifanya Kanda ya Ziwa iwe mikononi na kuua kabisa Sukuma gang, maana kazi anayoifanya Waziri Mkuu Majaliwa ilikuwa haihtaji msaidizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…