Kwa sasa kumekuwa na mmomonyoko mkubwa sana wa MAADILI hapa NCHINI ikiwa ni pamoja na Matumizi mabaya ya mitandao Kama kuweka picha na video chafu mitandaoni, ukahaba, umalaya, Matumizi ya madawa ya kulevya,ukatili wa kijinsia, Matumizi mabaya ya madaraka,ubadhilifu, utakatishaji Fedha, uhujumu uchumi yote hayo na mengine yanasabaishwa na ukosefu wa MAADILI pamoja na ATHARI ZA UTANDAWAZI.
Licha ya hatua kadhaa zilizochukuliwa na SERIKALI ikiwa ni pamoja na kuweka Sheria za uhujumu uchumi,utakatishaji Fedha,Sheria za maudhui mitandaoni,uanzishwaji wa mahakama za mafisadi,uanzishwaji wa madawati ya kijinsia lakini bado bado matukio yamekuwa yakiendelea kutokea kila kukicha hapa nchini
Sasa wakati umefika wa Serikali kupambana na changamoto hizi Kiroho na Kisaikolojia kwa KUFANYA SOMO LA DINI KUWA NI LA LAZIMA KUANZIA SHULE ZA AWALI HADI VYUONI, hii itwajenga watoto na vijana kufahamu kwamba kufanya matukio au matendo mabaya ni DHAMBI NA MAKOSA MAKUBWA KWA MUNGU kuliko hata kwa SERIKALI, hivyo itaisaidia NCHI katika KUKABILIANA NA MATUKIO OVU hapa NCHINI, vijana wengi wamekuwa wanakuwa KISASA ZAIDI bila kuwa na hofu ya mungu KABISA, hii ndo inapelekea matukio MABAYA KUENDELEA kutokea hapa NCHINI
Naamini SERIKALI ikiweka MPANGO MKAKATI katika hili SUALA litaleta ufanisi mkubwa Sana katika siku za USONI Kama likianza kufanyiwa kazi hivisasa.