Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile atenguliwa, Godwin Mollel achukua nafasi

Naomba tu nisaidiwe Jambo moja kwenye hizi Teuzi hivi Mtu Akitenguliwa mfano kuwa waziri au Naibu kama huyu.na Hajatiwa hatiani kwa kosa lolote na mahakama na hakuwa Idara yoyote selikalini Anaendelea kulipwa mshahara au vipi?? Au analipwa marupurupu yake kama mstaafu??au wanatemana naye anaendelea na maisha yake?? Maana idadi ni kubwa sana ya waliotenguliwa..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
haya tena lumekucha pale naona ..Dr.ndugulile anatolewa baada ya kupingana na maelekezo ya kocha wake na nafasi yake inachukuliwa na mchezaji aliyechukuliwa katika dirisha dogo la usajili baada ya kufungashiwa virago na mgt yake...na si mwingile Dr.Zwazwa....washabiki wanaonekana kutoridhika na hii sabu lakin ndo coach ameshaamua....
 
Mlisemaga sana mzee wa msoga anateua hadi dakika za lala salama.

Haya sasa.

Sent using iphone pro max
 
Hizo zilikuwa zama za mawe, boss kama kilaza tunakugalagaza tu.

Sent using iphone pro max
 
kwa taarifa tu Dr ndungulile ndio alikuwa kichwa kweny wizara si muongeaji ni mtendaji by professional ni daktari haswaa sio wa kuokota PhD kama humjui kaa kimya
hahaah jamaa anadhani ili mtu uwe mchapakazi ni lazima awe mtu wa kuongea ongea kwenye media or awe mtu wa maneno mengi ya uongo uongo bungeni huku umetoa na kukodoa mimacho kama yule profesa aliyeokotwa jalalani
 
Tuamtakia kila la heri huku mtaani na afuate maelekezo kutoka kwa wataalamu wa afya ya jinsi ya kujikinga na ugongwa huu wa COVID 19
upo na unaua.
 
Ila wanasiasa wa Tanzania muwe mnajiongeza kwanini msianze kujiuzulu kabla ya hizi tenguliwa?
Jiuzulu unamuacha mtu na aibu yake na kukujengea heshima ktk jamii.
Ujiuzulu hujipendi? Hukawii kutengenezewa ajali,ugonjwa au majambazi.
Ukiandika barua ya kujiuzulu,unashangaa barua ya utenguzi wako imepelekwa kwa Press na mwingine kateuliwa,kwenye "hansard" ya jamii inabaki "kuenguliwa".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…