Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt John Joseph Pombe Magufuli ( JPM) amtengua Faustine Ndungulile na kumuweka Dr. Mollel kuwa Naibu waziri Afya.
Ndungulile ni Mbunge wa Kigamboni, jimbo ambalo linaishi kama mtoto yatima.
Kigamboni ni sehemu nzuri sana kwa kuishi lakini kutokana na uongozi mmbaya wa huyu bwana, Kigamboni kuna ongoza kwa wizi tena ule wizi wa kuvamia majumbani.
Hajawahi kuonesha kuguswa na hili swala wala kuwajibika, what a shame!
Barabara za Kigamboni ni barabara kama za mbwa koko aliyekosa mfugaji. Napendekeza Jimbo la Kigamboni lichukuliwe na Kijana mdogo mwenye mission na vision ya kuifanya Kigamboni zaidi ya Osterbay kila mtanzania atamani kuishi huko.
Aidha; katika posti yangu ya uteuzi adhimu wa Mkurugenzi wa MSD, Brigedia Jenerali Grabiel Sauli Mhidize ( Dkt) nilisema wazi kwamba Hii chain ya kuanzia MSD; katibu Afya Zainabu Chaula alishaondolewa, Ndungulile nilisema nisehemu ya kuondolewa pia; hawa watu wamepewa nafasi kubwa kuliko uwezo wao. Faustine ni Dr. ni technical person ambaye anatakiwa kum guide Ummy na kumshauri vyema Waziri badala yake ameshindwa kuwa msaada kwa waziri.
Kuna Mtu yoyote anayejua kazi anayofanya Faustine? Tangu awe naibu waziri, je amefanya nini cha maana katika wizara hiyo ? I am Serious , zaidi ya kuposti kuwa watanzania wale matunda badala ya Tablets za Vitamin C!
JPM anania ya dhati na Wizara ya Afya; na amegundua kuna tatizo kubwa kwa hawa watendaji aliowaweka, napendekeza mabadiliko zaidi yafanyike. Hawa watu wametuangusha sana. Kwenye Afya hatutaki siasa, ni kazi kazi.
Je, MSD na Brig. Gabriel Mhidize, Itawezekana?
Je, MSD na Brig. Gabriel Mhidize, Itawezekana? - JamiiForums
Rais Magufuli amteua Brigedia Jenerali Gabriel Sauli Mhidize kuwa Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD)
Rais Magufuli amteua Brigedia Jenerali Gabriel Sauli Mhidize kuwa Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) - JamiiForums