Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile atenguliwa, Godwin Mollel achukua nafasi

Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile atenguliwa, Godwin Mollel achukua nafasi

Jambo zenu ndugu.
Naombeni kujuzwa ratiba ya kesho ya kuapishwa kwa huyu naibu waziri mpya aliyeteuliwa leo.

Sitaki kupitwa hata neno moja kwenye hotuba ya kesho, najua Kuna mabomu na makombora ya hatari yanategemewa kulipuliwa kwenye ukanda wote wa Africa mashariki na kusini.

Naombeni mda stahiki wajumbe, nasisitiza naombeni mda wa ratiba sahihi.
😂😂😂 Uwe na popcon kabisa.
 
Washauri wa mkuu ni tatizo aisee..huu ni zaidi ya uzwazwa!
Ni sawa na kumsimamisha kazi general na kumteua corporal kati kati ya vita ni dharau kubwa mno sio kwa raia tu bali hata kwa morale ya wafanyakazi wa afya kipindi hiki ambacho wanahatarisha usalama wao kumuweka mtu atakaekuja kuongea ujinga wakati madokta huko wanajitoa muhanga na hakuna mtu wakuwasemea wanacho deal nacho.
 
Mpendwa Mteja, tunakusihi endelea kujifukiza na kufuata maelekezo ya Wataalam kuhusu namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya #CORONAVIRUS. Aidha, tunakushauri kuepuka kusikiliza taarifa zisizo sahihi kutoka vyanzo visivyoaminika
 
Ndungulile alitaka sayansi itawale na sio ujinga wa nyungu sijui kujifukiza ambako hakuna ushahidi wa kisayansi kama kunatibu ugonjwa. Hii iko kinyume na matakwa ya boss anaetaka ujinga ndio utumike kama tiba ya corona.

Ndungulile hakupigia debe matakwa ya bosi wake ya kutumia tiba za kienyeji.View attachment 1452150

Kwenye kitabu cha Robert Greene cha 48 rules of power, Rule namba moja inasema never out smart your master. Always make them feel or appear more brilliant than he is. Always make your boss feel intelligent than you.

Ndugu yangu Ndungulile utakua ulisahau hili.
Hii imekaa sawa sawa..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee wa vijembe! Ameshakuwa predicted, akitaka kuita press conference ya kujibu vijembe na udaku lazima atumbue mtu na aapishe ili apate attention ya watu na media.
Mulemule..Ni Akili ya Ovyo sana
 
Hivi hii wizara ilikuwa na naibu waziri? Mie nilijua ni kama wizara ya Katiba na Sheria ambayo inawaziri tu. Maana namsikiaga Ummy tu. Huyu Ndungulile alikuwa anahusika na shuguli gani, ili tuone pengo atakaloliacha?
kwa taarifa tu Dr ndungulile ndio alikuwa kichwa kweny wizara si muongeaji ni mtendaji by professional ni daktari haswaa sio wa kuokota PhD kama humjui kaa kimya
 
Ni kweli kabisa, lakini ukumbuke huyo head anasubiri ushauri wa kitaalam kutegemea nini anaongoza. Huoni ni added advantage kama yeye pia anayo professionalism ktk hiyo nyanja..???


Hapo kwenye taaluma, administrative siyo lazima top leader wa organisation flani kuwa mwenye taaluma inayoendana na kile anachokiongoza ndo maana unaona Mwigulu yupo kwenye katiba na sheria japo kasoma uchumi n.k hiyo haina shida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom