TANZIA Naibu Waziri wa Elimu Mstaafu Mzee Nazar Nyoni afariki dunia

TANZIA Naibu Waziri wa Elimu Mstaafu Mzee Nazar Nyoni afariki dunia

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Naibu Waziri wa Elimu wa zamani wa Serikali ya Tanzania wa Awamu ya Kwanza, Mzee Nazar Nyoni, amefariki dunia jana tarehe 19/07/2024 majira ya saa 3 asubuhi nyumbani kwake Morogoro baada ya kuugua kwa muda mrefu. Mzee Nyoni amefariki akiwa na miaka 92.

Marehemu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Elimu wa Tanzania kati ya mwaka 1975 hadi 1980 na ametoa mchango mkubwa katika sekta ya elimu nchini Tanzania. Alifanya kazi kwa karibu na serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya Hayati Julius Nyerere.

Mazishi yatafanyika Jumatatu tarehe 22/07/2024 Kola, huko Morogoro.

Screenshot_20240719_222331_WT Hub.jpg

Chanzo cha taarifa hii ni mwanafamilia. Tunatoa pole kwa familia, marafiki na wote walioguswa na msiba huu.
 
Asante kwa taarifa hii, wakati akiwa. Naibu Waziri, nimesoma primary na watoto wake wawili wa kiume, mmoja akiitwa Paskali, jina lilikuwa Nizar Nyoni, kumbe ni Nazar!

Waziri wake alikuwa Tabitha Siwale.
RIP Waziri Nyoni.
P
Classmates zako hao wamefiwa na baba yao, watafute uwape pole....mkuu
Huwa nalikumbuka tu swali lako kwa mwendazake....
 
Back
Top Bottom