Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Naibu Waziri wa Elimu wa zamani wa Serikali ya Tanzania wa Awamu ya Kwanza, Mzee Nazar Nyoni, amefariki dunia jana tarehe 19/07/2024 majira ya saa 3 asubuhi nyumbani kwake Morogoro baada ya kuugua kwa muda mrefu. Mzee Nyoni amefariki akiwa na miaka 92.
Marehemu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Elimu wa Tanzania kati ya mwaka 1975 hadi 1980 na ametoa mchango mkubwa katika sekta ya elimu nchini Tanzania. Alifanya kazi kwa karibu na serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya Hayati Julius Nyerere.
Mazishi yatafanyika Jumatatu tarehe 22/07/2024 Kola, huko Morogoro.
Chanzo cha taarifa hii ni mwanafamilia. Tunatoa pole kwa familia, marafiki na wote walioguswa na msiba huu.