Naibu Waziri wa Maji aagiza fundi wa mradi awekwe ndani

Naibu Waziri wa Maji aagiza fundi wa mradi awekwe ndani

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Huyu ni naibu waziri wa maji, Meryprisca Mahundi.

Baada ya kuchukizwa na kitendo alichokifanya fundi Imani Mussa, ambaye ni fundi wa mradi wa maji huko Kyenda, wilaya ya Ngara, mkoani Kagera.

Inadaiwa fundi alitaka kuupeleka msafara wa Bi. Naibu waziri kwenye sehemu tofauti na sehemu iliyo na changamoto.

Baada ya Bi. Naibu waziri kugundua hilo, akaagiza fundi huyo kushikiliwa na polisi.



My first take:

Ukali katika utendaji kazi ni kitu muhimu katika kufanya shughuli ziende.

Tanzania huwa kuna uzembe wa kipumbavu sana.

Mimi mwenyewe nimeshawahi timua mafundi [wa kienyeji] kadhaa kwa uzembe.

Kuna mmoja aliwahi kuniambia eti alisahau kama asubuhi alikuwa na kazi ya kufanya kwenye ka mradi kangu licha ya kumpa ‘advance’ jana yake.

Aliponiletea habari za kusahau, nikamtimua maana hakuwa serious. Na fundi asiyeichukulia serious kazi yake, hata kazi atayokufanyia, yaweza isiwe ya kiwango unachokitaka wewe.

Nikija kwa huyu Bi. Naibu waziri, ni kweli anayo mamlaka ya kuagiza mtu awekwe ndani? Anayatoa wapi hayo mamlaka? Hajavuka kweli mipaka ya kazi yake?

Kwa mnaojua, tuelimisheni tusiojua.

Mimi naona ingekuwa ni vyema zaidi kwa Bi. Naibu waziri kumtimua kazi huyo fundi moja kwa moja au kuongea na mwajiri wa huyo fundi na kumshawishi amtimue kazi.

Siyo kuagiza awekwe ndani.

What say you?
 
Inapaswa tuwe na mwendo wa Aina hii ya Ki JPM kama miaka 20 ijayo, iko faida

Nachomwomba Mungu atuandalie tena mtu wa mfano wa JPM baada yake!!
 
Inapaswa tuwe na mwendo wa Aina hii ya Ki JPM kama miaka 20 ijayo, iko faida

Nachomwomba Mungu atuandalie tena mtu wa mfano wa JPM baada yake!!
hatokuja kama yeye. just tuombe anaekuka aendeleze hii miradi. asije na project zake zingine tukaanza A
 
Mambo ya kishamba haya. Kufanya kazi kupitia media.
 
Mimi naona katika wizara zinazofanya vizuri ni hii ya maji
 
Naibu waziri naye fala tu, atakwendaje na fundi kukagua mradi? Naibu waziri alitakiwa kwenda na meneja wa Ruwasa ambaye ndiye anawajibika na ujenzi na uendeshaji wa miradi yote ya maji wilayani.
 
Back
Top Bottom