Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Baadhi ya wadau walikuwa wanajiuliza kwamba kama Waziri wa Mambo ya ndani na Katibu wake wameng'olewa mbona wasaidizi wao hawajaguswa ?
Jibu laweza kupatikana baada ya Naibu Waziri wa mambo ya ndani Hamad Masauni na Naibu Katibu Mkuu Ramadhan Kailima kutinga TAKUKURU kwa mahojiano .
Dodoma. Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Ramadhan Kailima leo asubuhi Februari Mosi, 2020 amefika katika ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mjini Dodoma kuhojiwa.
Kailima amefika katika ofisi hizo kuhitimisha idadi ya walioondolewa kwenye wizara hiyo na wanaoendelea na majukumu yao kuhojiwa na taasisi hiyo kwa agizo la Rais John Magufuli.
Jana alihojiwa aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Kangi Lugola, Meja Jenerali Jacob Kingu (alikuwa katibu mkuu) pamoja na aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye.
Mbali na Kailima, naibu waziri wa wizara hiyo, Hamad Masauni naye atahojiwa leo.
Wote wanatuhumiwa kuhusika katika mkataba wa jeshi la Zimamoto unaotajwa kuwa na harufu ya ufisadi. Rais Magufuli ndio aliibua kasoro katika uingiaji wa mkataba huo na kuwataja jinsi walivyohusika.
Magufuli amesema Kailima alihusika kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mchakato wa kuingia mkataba huo wa kununua ndege zisizo na rubani kwa ajili ya kuzima moto. Kiongozi mkuu huyo wa nchi amesema Kingu aliandika barua ya kujiuzulu na kuiridhia. Kingu ameteuliwa kuwa balozi.
Kailima amewasili Takukuru saa 2:52 asubuhi katika gari aina ya Toyota Land Cruiser.
Huku akiwa amevaa tisheti ya mistari ya rangi nyeupe na damu ya mzee na suruali nyeusi, alikuwa ameambatana na msaidizi wake aliyekuwa amebeba begi jeusi.
Baada ya kushuka katika gari hilo, aliingia ndani kupitia mlango mdogo wa ofisi hizo, baada ya muda alitoka na kupita katika mlango mkubwa ambao ndani kuna eneo la mapokezi.
“Jamani salama,” amesema Kailima wakati akipishana na waandishi wa habari waliopo ndani na nje ya jengo hilo lililopo mtaa wa Jamhuri.
Pia soma: Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola adaiwa kuwa chini ya ulinzi
Kangi Lugola aripoti ofisi za TAKUKURU Dodoma kwa mahojiano
#HABARIZAHIVIPUNDE:Aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani Kangi Lugola asubuhi hii, ameitikia wito wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani Dodoma, ambapo amewasili katika ofisi za TAKUKURU saa 1.24. ===== Dodoma. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola...