Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni na Ramadhani Kailima watinga TAKUKURU kuhojiwa

Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni na Ramadhani Kailima watinga TAKUKURU kuhojiwa

Unaousema ndio ukweli. Katika sakata hili, Masauni alilaumiwa na Rais pia. Siyo yeye tu, hata Naibu Katibu Mkuu (Kailima) pia alilaumiwa na Rais pia. Lakini Masauni na Kailima wameendelea na kazi kama kawaida! Hiki kitu nilijiuliza mwenyewe japo zikuanzisha uzi hapa JF.
Wala siyo Masauni aliyemtonya Rais,kama unakumbuka Rais pia alimlaumu Masauni kwamba alisikia japo hakuhusishwa ila alikaa kimya. Ninaamini kabisa kama jamaa angemtonya Rais moja kwa moja baada ya kusikia angepewa wizara.
 
Baada ya wiki boss wa TAKUKURU akaja kwa fujo kuwa upelelez umekimilika hivyo wiki ijayo kangi na mwenzake watafikishwa mahakaman....kkmyaaaaa hadi leo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka katika lile sakata la mkataba wa kununua vifaa vya kuzima moto lililopelekea kutumbuliwa Kangi Lugola na Kamishna Thobias Andengenye, Mheshimiwa Rais Magufuli alisema Naibu Waziri alishaandika barua ya kuachia ngazi mapeema na hata akashangaa Waziri alipataje guts za kuhudhuria kwenye mkutano wake.

Leo nilikua napitia magazeti katika mtandao nikakutana na habari za Masauni akiwaagiza polisi huko Zanzibar kuwaachia kwa dhamana watuhimiwa wenye makosa ya kudhaminika ili kujikinga na maambukizi ya virusi ya korona.

Sikumbuki kusikia kauli ya kumrudisha kwenye nafasi yake lakini nikiri pia sikuwahi kumsikia Mheshimiwa Rais akisema amekubaliana na barua ya kujiuzulu la Masauni

Kwa muktadha huo najiuliza je Bwana Masauni sio miongoni mwa waliofanya kazi ya kum snitch Kangi na Thobias huku ikionekana na yeye naye yupo kwenye hot soup lakini kiuhalisia yeye ndio kauza wenzie?

View attachment 1414743
Mi huwa nashangaa siku zote mawaziri au naibu Waziri wenye nasabu kutoka Zanzibar hawaguswi na kashfa za kifisadi ...sijui labda ni wasafi zaidi ya malaika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wala siyo Masauni aliyemtonya Rais,kama unakumbuka Rais pia alimlaumu Masauni kwamba alisikia japo hakuhusishwa ila alikaa kimya. Ninaamini kabisa kama jamaa angemtonya Rais moja kwa moja baada ya kusikia angepewa wizara.
Ndiyo hivyo, rais alisema alikuwa anapokea vi memo tu baada ya wakubwa kufanya yao, na akawa anamwambia kwanini hakumtonya rais, unajua wengi hatupendi kusikiliza mpaka mwisho tunakuwa yanaendelea busy for nothing muda wote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo hivyo, rais alisema alikuwa anapokea vi memo tu baada ya wakubwa kufanya yao, na akawa anamwambia kwanini hakumtonya rais, unajua wengi hatupendi kusikiliza mpaka mwisho tunakuwa yanaendelea busy for nothing muda wote

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndiyo uache umbeya, utagongwa bure kudandia gari kwa mbele

Sent using Jamii Forums mobile app
Suala la umbeya linatoka wapi tena wakati Masauni alishaandika barua ya kujiuzu na hakuna mahali popote ambapo Mheshimiwa Rais alisema hajakubali barua yake ya kujiuzulu?. Unafahamu pia kujua uhalifu unatendeka na kushindwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika ni kosa pia?

Rais amemfanyia favour kuendelea kumuacha hapo. Wanaosema Masauni ndio alikua whistle blower je ilikua ni kabda au baada ya Katibu Mkuu kumueleza Rais?
 
Sikuwahi kuiskia hiyo kauli mkuu. Ninachokumbuka siku ile kwenye ile hafla ya polisi pale kurasini Rais alisema Naibu Waziri alisha achia ngazi kwa kupeleka barua ya kujiuzulu na akawa anamshangaa Kangi kwa ujasiri wa kuhudhuria hafla ile kwani hakutarajia kumkuta pale! Sikumbuki kumsikia akisema amekataa kujiuzulu kwa Masauni
Mkuu huyo jamaa unayejibu comment yake yupo sahihi.

Masauni hajatumbuka wala kutumbuliwa.

Ukitaka ukweli, tafuta clip ya msingi ya ziara hiyo ipo mitandaoni ili kumaliza sintofahamu uliyonayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama utakumbuka vizuri Rais alisema KM alimfuata akamueleza uozo unaoendelea pale Wizarani kuhusiana na huo mkataba na hakutaka kua sehemu ya huo uchafu na akaomba kujiuzulu na Rais akasema atamuheshimu sana kwa uamuzi wake huo

Kuhusu Naibu Waziri, Mheshimiwa alisema tu "Ameshaandika barua ya kujiuzulu na hapa hayupo, nashangaa kukuona hapa Waziri!"

Ila nikiri pia sikumbuki kama katika walioitwa kuhojiwa TAKUKURU na NW alikuwepo
Huyo alikuwa ni katibu mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom