Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tutatumia VPN wakipiga ban.Imevujisha desa kwamba mitandao hii mnayoitumia inakwenda kuougwa ban muda si mrefu
Hivi hawa watu wana matatizo gani....
Lazima kuna tatizo mahali si bure...
we think alike.
So far comments zote zimemponda nashangaa.
Hivi kila nchi ikianzisha social media zake hali itakuwaje? kwanza ni kwa kiwango kidogo sana sisi tunatumia social media kwa mambo ya maendeleo, mtu anayefahamu vzr IT kwa nchi kama yetu kipaumbele ni ku-leapfrog kwenye IT itusaidie kutatua changamoto nyingi kiuchumi, kijamii..afya, kodi, kilimo, elimu, sanaa nk, yote haya waziri hajui, anachojua ni kuanzisha twitter, whatsap, youtube za kwetu..aanzishe yeye kwanza kama anaona italeta maslahi kwa nchi na kwake.Mwambe mwenyewe ameshindwa hata kujibrush ule mwonekano wake angalau umpe haiba ya Leader, mfano afuge hata mandevu tu, au aache nywele ndefu aka afro...always looks like mwanachuo tena mwaka wa kwanza first degree, uongozi ni haiba pia, ule mwonekano wa nje ndio unajenga kuaminiwa kabla hujasema neno, lakini wakati mwingine tatizo si Mwambe, tatizo ni waliomuona na kumpa hizo nafasi hao ndio tatizo pengine kuliko hata Mwambe, factor wanazotumia kumsaidia mteuzi ni dhaifu sana, kama ufaulu wa chuo ndio kigezo, kwenye zama hizi basi bado tuna safari ndefu sana kupata watu wenye uwezo kutatua changamoto tulizo nazo...ni ajabu Mwambe kupewa uwaziri wa viwanda tena ni first timer bungeni wanaachwa kina Bashe ambao tayari walikuwa wameonyesha uwezo kwny wizara walizokuwa...tuna kasoro kubwa sana kwenye vetting process iliyopo. Inawezekana tanzania tu, mtu anateuliwa siku ya siku anashindwa kusoma kiapo, kapitishwa pitishwa kote huko...mara Uded, mara kagombea ubunge mara ya kwanza kashindwa, mara ya pili kashindwa tena lakini akabebwa, unaona kabisa kuna watu wana bebana bebana tu, juzi naibu waziri wa teknolojia, Kundo wa hii wizara mpya, anahojiwa na media kitu gani kwny teknolojia anadhani kina mchango kwny maendeleo yetu...anasema inabidi tuwe na Instagram kwa lugha yetu, tusitegemee za wenzetu, fikiria huyo ndio waziri anasema hivyo, kwake kitu cha maendeleo kinachotrend akilini mwake ni kuwa na instagram zetu wenyewe hiyo ndio priority kichwani mwake, waziri wake Dr. Ndugulile baada ya kushindwa kwenye wizara ya afya wakati akiwa naibu tena kwenye fani yake, leo unampa wizara mpya ambayo hata si fani yake, unawaacha kina Profesa Mbarawa waliofanya vizuri term iliyopita angalau...ni mengi ya hovyo kabisa kuyasikia, sema tu sisi watz akili yetu ni nyepesi sana siku zote haitaki kuangalia mambo yanayofanyika kwa kina kujua kama yanatufaa au hayatufai...tatizo lipo kwa wanaomsaidia mteuzi, wao kwanza ndio walipaswa kushughulikiwa kabla ya kuwalaumu wanaoteuliwa!