Naibu Waziri wa TEHAMA, Kundo Andrea ashauri TCRA kuanzisha mitandao yetu ya kijamii tuachane na Twitter, FB, YouTube n.k

Naibu Waziri wa TEHAMA, Kundo Andrea ashauri TCRA kuanzisha mitandao yetu ya kijamii tuachane na Twitter, FB, YouTube n.k

Mimi ningewashauri wangetengeneza mtandao wa kukusanya kodi kwanza usiwe kila siku uko down walipa kodi wanacheleweshewa huduma na serikali wanachekeweshewa malipo!
 
Kha

FB_IMG_1611162362590.jpg
 
Malaika wa mitandao ameanza kushuka kwa dizaini fulani.
 
Hajui maana yake. Ingekuwa raisi hivyo mzee baba TRUMP na ebilionea wake angeanzisha yake baada ya hizo social media kumpiga BAN. Sio kazi nyepesi ya uwekezaji. Uliza google ndo atajua hasichokijua hicho
 
Wazo la kila mwananchi kupata maji tiririka lisubiri mpaka Lissu akiwa Rais.
 
Muwe mnachungulia tunaongea nini? tuuze mahindi ya kuchoma tu na mihogo tuko vizuri.
 
JF tu inapigwa vita hivyo ndio aje na mitandao yake? Maybe alimaanisha mitandio sio mitandao
 
Tanzania ni kama Mtu asiye na pesa halafu ni limbukeni! Anajikweza ili na yeye aonekane yupo
 
hii nayo pumba nyingine.

katika nchi ambayo hakuna uhuru wa vyombo vya habari wala wa kutoa maoni unategemea serikali ianzishe social media watu waziamini?

facebook, instagram, twitter ni social media za kimarekani nchi ambayo uhuru wa habari na wa kutoa maoni vinathaminiwa, kulindwa na kuheshimiwa.

hakuna uhuru nchi hii kwa hiyo bwana naibu waziri katema pumba.
 
Labda kama tutatumia Satellite internet ya kichawi kuendeshea hiyo mitandao. Anazani vitu ni rahisi rahisi km kuwaonea Chadema!
 
Chonde chonde... Msiingie huko mtaharibu na mtatutesa bure...

Malizeni kwanza matatizo ya maji, mashule, umeme, mahospitali, barabara nk. Huko kwingine mkigusa (haijalishi ubora mtaokuja nao) mtavuruga tu... Mtaishia kuchuja content na kulazimisha mapambio tu ndo yasikike na yachukue % kubwa ya content ya hizo social media za kisiasa.
 
"Natamani malaika washuke wayafunge mitandao ya kijamii walao mwaka mmoja"- JPM
 
Nikisoma between the lines kama kuna kitu anataka sema...

Ngoja niunge doti..

China mpaka leo whatsapp imepigwa ban, google na fb nadhan hazipo pia!!

Je tunataka fwata nyayo za china?

Ke haya yote yanawezekana vipi kwenye huu mfumo mbovu wa elimu ambao injinia wa kompyuta hawezi hata kuunda website?

Huyu mtu sio wa kumdharau... kuna kitu kipo!!

NB: JamiiForums ni mtandao wa kitanzania na mpaka sasa una kesi mhakamani iliyo funguliwa na serikali.
Dah
 
tuwe na Facebook, Instagram, twitter yetu itafanya uchumi wetu kuwa stable na tutakuwa tumeimarisha usalama wa nchi yetu" Eng. Kundo
Such useless thinking of our time by our own leaders. Kwani Facebook, Twitter, et la zilianzishwa na Serikali au mashirika ya umma!?
Nope! Unatarajia temesa, tanroads, tba au Suma JKT kuwa vitovu vya innovations kwenye arena ya ICTs? Nope! Useless thinking of our poor leadership!
 
Back
Top Bottom