Naibu Waziri wa TEHAMA, Kundo Andrea ashauri TCRA kuanzisha mitandao yetu ya kijamii tuachane na Twitter, FB, YouTube n.k

😁😁😁😁 uchumi wa social media kutoka uchumi wa viwanda.
 
Amenifurahisha sana hapo aliposema Facebook, twitter & YouTube zikiblockiwa hapa Bongo makampuni ya simu yatapata taabu sana.

Kumbe hata serikali kwa namna moja ama nyingine inategemea sana kodi inayopatikana kutokana na hii mitandao ya kijamii ya ubeberuni
 
Serikali inatoa go-ahead watu mnasema bangi sio nzuri.
Sasa aje mtu aongee umbea humu Ooh! I am a programmer, I have no life, mara Ooh Nimesoma IT naomba connection.


Mimi nitakuwa wa kwanza kukomenti kikatili juu ya mtu huyo.

Fanyeni Programming na mtuletee mitandao ya kijamii Kama Jamii Forum na mkapate mkate wenu huko.
 
Yani watu mnafunga ili Maxence wa JF mumpeleke jela, yani hapa kodi mpaka kuongea
 
Tunayo JF, itakayo anzishwa kama japo tu ikiwa na faragha kiwango cha facebook hata shetani atapongeza hatua hiyo kwani media na uhuru w a habari kwetu ni sumu.
 
Hiyo mitandao itakayoanzishwa na wanaccm watatumia wanaccm wenyewe.
 
Hivi hawa watu wana matatizo gani....
Lazima kuna tatizo mahali si bure...

kila siku tunasema wapumbavu ni wengi sana Tz hamwelewi ...yan waanzishe mashindano na magiant kama twita na fecbook ahahaha kazi ipo kwakweli
 
Nimemuelewa injinia. Ni kwamba:-

1. Mitandao ya nje wataishut down.

2. Kutakuwa na server ya aifa ambayo wataweza kui-access.

3. Hakuna kutumia majina yasiyo halisi.

4. Kuna ishu kaongea kuhusu innovation.

Big brother is watching you.
 
we think alike.
So far comments zote zimemponda nashangaa.

Mkuu yupo very wrong mzee hata kama kuna sehemu anapointi, yan its like wanataka waanzishe kitu kama tbc , yan kitu ambayo they will have full control in all the necessary means, sasa what are they trying to achieve?

Nimejaribu kuwaza motive yao nimeona ni vitu vya kipuuz tu, kama kuanzisha you tube channel tu mtu mpaka ulipie hela ivyo vingine itakuwaje ??

Kwanini hawa jamaa wa madarakan wanaogopa sana criticism ?

...Mkuu nakuhakikishia something somewhere is not okay...
 
Huyu waziri ni kama anachofikiri ni hiki tu, kwa mara nyingine amerudia tena maneno haya..yeye sasa ni consultant anaelekeza nini wengine wafanye, sifahamu kwa nini alishindwa kujaribu hayo anayoishauri TCRA wakati hajawa waziri..mara ya kwanza aliposema, nilidhani atajirekebisha baada ya kusoma hapa..
Hivi kila nchi ikianzisha social media zake hali itakuwaje? kwanza ni kwa kiwango kidogo sana sisi tunatumia social media kwa mambo ya maendeleo, mtu anayefahamu vzr IT kwa nchi kama yetu kipaumbele ni ku-leapfrog kwenye IT itusaidie kutatua changamoto nyingi kiuchumi, kijamii..afya, kodi, kilimo, elimu, sanaa nk, yote haya waziri hajui, anachojua ni kuanzisha twitter, whatsap, youtube za kwetu..aanzishe yeye kwanza kama anaona italeta maslahi kwa nchi na kwake.
 
Ndio mapungufu ya mfumo wa elimu ya Tanzania, kukusanya vyeti (vertical knowledge-elimu ya makaratasi) horizontal knowledge zero..hivi kweli mtu mwelewa anaweza amua ku-swim kwenye kina cha maji kimejaa mapapa damu imetapakaa akidhani anaweza kuogelea na kufika anakotaka kwenda? sijui..
 
...mnisaidie 4.10 zile nanilii maana yake nini? walimuacha Mzee Chenge bure tu, km mambo yenyewe ndio nanilii..
 
Kubadilisha vitabu vilivyoandikwa teyari na wazungu ila kazi yao iwe ni kunakili tu kutoka kiingereza kwenda kiswahili mpaka leo wanashindwa. Sasa ili ni nje ya uwezo wetu nafikiri.
 
Naunga mkono hoja!
Najua contractors wa facebook,Twitter, na instagram 'mnafuka moshi' kwenye uzi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…