Naifurahia sana fani yangu ya upishi

Naifurahia sana fani yangu ya upishi

Zikinata inamaana umezidisha maji au haujazikanda zikakandika. Endelea kukanda hadi donge liwe lainiiii.

Mi naacha bhana wee,cha kujifia 😂😂😂
 
Hii ni mara ya kwanza kupika chapat baada ya kujifunza kupika youtube na hakika nmeweza laini mno,sipat picha kwa mara ya pili itakuaje
20200316_201221.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chapata kuwa ngumu sana tatzo ni mafuta au maji...?

Mana juzi nmejaribu tatzo Kama ilo limetokea nikahisi labda maji niliweka kidogo...adi naogopa kupika chapata za kusukuma Mana sku ile niliharibu unga wa bimkubwa alimind sanaa

Chapati kuwa ngumu ni matokeo ya ukandaji na uchomaji process yote kwa ujumla. Unaweza kuwa umenyima mafuta, au umenyima maji wakati wa kukanda au dough halijaivaa (umekanda unga haujalainika vizuri).

wakati wakuchoma yawezekana umenyima mafuta, au umechomea moto mdogo sana au umechomea moto mkubwa sana, haya yote kwa pamoja yanaleta matokeo ya chappo ngumu.

Ni rahisi sana hasa ukishajua ukandaji, kukunja chapati na kuichomea moto wa wastani utakuwa unafanya chapati laini hadi unapenda mwenyewe.. kujiimarisha zaidi tumia samli,au cowboy kwenye kukanda, kuongeza ladha kandia maziwa ya unga, au nazi.
 
Kiasi kingi cha unga nilichowahi kupika ni nusu kilo...mara nyingi napika robo kilo,sasa hapa sijui natakiwa kuweka chumvi kiasi gani?

Nikionja nikaona chumvi ni nyingi naipunguza kwa namna gani?

Kwenye kukanda inawezekana ikawa ni tatizo kwasababu nikiangalia youtube namna dough inavyokuwa na nikiangalia ya kwangu ni tofauti,za youtube ziko katika namna ya kuvutika hivi while niliyokanda mimi inakuwa inakatika katika....hapa huwa nashindwa kujua tatizo ni uwingi/uchache wa maji na mafuta ama nakosea kwenye kukanda?
Unakosea kwenye kukanda...

Na unaweka unga mwingi kwa wakati mmoja especially kama unatumia mkono kukanda. Weka unga kidogo kidogo. Dough inatakiwa iwe smooth kama ugali. Kwani ugali ukipika huwa unaacha mabongemabonge?

Nusu weka 1 teaspoon...ijae. pia kama ukadiriaji wako wa chumvi ni tatizo weka kidogo kidogo huku ukionja. Kwanini uweke nyingi kwa mpigo.

Mimi chumvi nawekea kiganjani bila kipimo maalum na siwezi kukosea.

Tatizo lako kubwa ukandaji. Weka unga kidogo kidogo huku ukihakikisha umekuwa laini na wa kuvutika. Kabla ya kukata balls zako weka tena mafuta kiasi kanda tena hadi mafuta yaingiliane na unga. Baada ya hapo anza kukata balls zako.
 
Nitajaribu hii mara ya mwisho,nitakupa mrejesho baba naniliu
 
Chapata kuwa ngumu sana tatzo ni mafuta au maji...?

Mana juzi nmejaribu tatzo Kama ilo limetokea nikahisi labda maji niliweka kidogo...adi naogopa kupika chapata za kusukuma Mana sku ile niliharibu unga wa bimkubwa alimind sanaa

chapati kuwa ngumu yawezekana wakati wa ukandaji hukukanda unga vizuri, au baada ya kukanda hukuaacha walau dakika 20 zile za kuupa nafasi kulainika vizuri, au wakati wa kuchoma ulichoma na mafuta meengi ama mafuta kidogo ndo maana zikawa ngumu.

hivyo ili kugundua hilo next time jaribu kua makini
ukiwa unakanda kanda unga ulainike vizuri then uache kwa dakika kadhaa ata 20 au nusu saa unasaidia kulainisha zaidi, then wakat wa kuchoma hakikisha huzidish wala hupunji mafuta, moto usiwe mwingi usiwe mdogo..

Au try this way wakati wa kukanda weka walau vijiko viwili au vitatu vya maziwa mtindi itasaidia chapati zako zitakua laini, zitachambuka na taste yake ni nzuri mnooo (ila uwe makini usiweke maji mengi sana )

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uje nikufundishe mdogo wangu....... andaa zawado nono ya kunitunuku.
Mie nikija nakuja kula tu, sitaki kujifunza maana nikishajua nitapata shida kupika. Kwasasa najua kuchemsha chai tu hiyo inatosha.
 
Back
Top Bottom