Naingia Shambani very serious kulima Alizeti

umechelewa sana mkuu
ilibidi oale pale scarcity ya cooking oil ilipotokea ungefanya maamuzi.wengi wanaotamba na alizeti kwa sasa ni wale waliohifadhi alizeti kwenye maghala kusubiria demand iwe high and sure this time hesabu imeangukia uoamde wao
 
Mi nalima tu
Na kukusanya alizeti toka kwa wakulima

Hapa nachakata akili Kama nikamue au nihifadhi

Kwa hali ilivyo na uhitaji nakushauri ukamue tu
Kuna mashine ndogo China za kukamua it won’t cost you a [emoji3091]
 
Duh hii thread imenifanya nipate hamu ya kulima alizeti japo sijawahi kujaribu mtaji sina ila hivi nikitafuta 2M kwa kuanzia ikawa ndo gharama ya kwanzia kukod shamba had kuvuna ntakua nipo chini sana au standard
 
Mi nalima tu
Na kukusanya alizeti toka kwa wakulima

Hapa nachakata akili Kama nikamue au nihifadhi

Kama upo jirani na mashine nzuri za kukamua basi kamua uhifadhi mafuta
Kuhifadhi Alizeti yenyewe ni gharama na panya wasumbufu
 
umechelewa sana mkuu
ilibidi oale pale scarcity ya cooking oil ilipotokea ungefanya maamuzi.wengi wanaotamba na alizeti kwa sasa ni wale waliohifadhi alizeti kwenye maghala kusubiria demand iwe high and sure this time hesabu imeangukia uoamde wao

Kwasasa watu wanavuna alizeti bei lazima itashuka

Ukitaka kufanikiwa kwenye mazao ya nafaka inabidi uwe mvumilivu kwa kuhifadhi na kuja kuuza msimu unapokwisha na bidhaa kuadimika
Lakini kama unalima kisha utegemee kuuza ukivuna tu lazima itakupa changamoto ya bei kuwa chini

Hakuna kuchelewa ni timing tu
 
Duh hii thread imenifanya nipate hamu ya kulima alizeti japo sijawahi kujaribu mtaji sina ila hivi nikitafuta 2M kwa kuanzia ikawa ndo gharama ya kwanzia kukod shamba had kuvuna ntakua nipo chini sana au standard
Kwa hiyo pesa hukodi kulima kuanzia heka 15
 
Kama upo jirani na mashine nzuri za kukamua basi kamua uhifadhi mafuta
Kuhifadhi Alizeti yenyewe ni gharama na panya wasumbufu

Bei imeshuka 5lita ni 25,000

Nadhani mpaka June itafikia 18,000

Ila later on itapaa kwa sababu hatuna uhakika wa importation ya mafuta mpaka sasa
 
Bei imeshuka 5lita ni 25,000

Nadhani mpaka June itafikia 18,000

Ila later on itapaa kwa sababu hatuna uhakika wa importation ya mafuta mpaka sasa
Kweli kabisa mkuu

Haya mazao ukisema uuze msimu wa mavuno bei inakua changamoto
Hapo ni mwendo wa kupiga stock tu bei itakaa vizuri baadae sana
 
Imefikia 90,000 Ila kutatokea shortage very soon Kenyans wananunua Kwa Kasi.
Unalima wapi ww ndugu... nataka kulima hiyo kitu ila sijapata sehem nzuri... nina trekta nataka shamba tu
 
Aisee...
Sasa kama ulilima ndio unapiga hela hasa....na hii vita
 




MREJESHO WA MWISHO

GHARAMA za MAVUNO
Kuvuna Eka 20 x 30,000 = 6000,000
Kupiga na kupeta kwa mashine 1000 kwa gunia = 92,000
Mifuko. 50,000 500 kwa mfuko
Usafiri 100,000
Vibarua na mengineyo 100,000

Jumla 1,000,000

Ukichukua gharama za awali kuanzia kukodi shamba, mbegu, kulima, palizi nk jumla ilikua 4,500,000
Ukijumlisha na hii ya uvunaji 1,000,000 jumla kuu ya GHARAMA ZOTE INAKUA 5,500,000

MAVUNO
Nimepata jumla ya gunia 92..........wastani wa gunia 4.6 kwa eka

Kwa sasa gunia la alizeti linauzwa 90,000(i hope litafika 150,000)

Nikisema niuze sasa maana yake ni
90,000 x 92 = 8,280,000

Kukokotoa Faida/hasara

Mauzo. 8,280,000
Gharama 5,500,000

8,280,000-5,500,000 = 2,780,000 FAIDA

Kwa sasa sina mpango wa kuuza alizeti wala kukamua
Nitaiweka stock hadi itakapo adimika bei itakua nzuri na mashudu yatakua bei juu pia
Kwa muda huu naanza kununua rasmi alizeti angalau gunia zingine 250 au 300 ili bajeti yangu ya 40m isogogee kidogo, kisha nitakuja kukamua na kuuza mafuta......nimekamua gunia moja nimepata lita 20 na point
Dengu nimeshindwa kulima sababu ya nvua mbuga imekauka sana

Namshukuru sana MUNGU na wote mlionipa moyo na hata walio nikatisha tamaa kwani walinipa chachu zaidi

Kikubwa nilicho jifunza kwenye kilimo ni usiwe mbahili kwenye mambo ya kitaalamu....... fuata exactly wataalam wanavyo shauri haswa kwenye
Muda wa kulima mapema
Kupanda kwa kanuni
Kupalilia kwa wakati
Uvunaji kuzuia kupoteza mazao mengi on process
Na mwisho simamia mwenye kila hatua

Kwa muda niliotumia na faida iliopo hadi sasa sio kubwa lakini kwangu mimi ni USHINDI mkubwa sana kwa maana ya UZOEFU
(Iwapo bei itafika 150,000 kama msimu uliopita basi nategemea kuuza 11m faida itakuja 5.5 sio mbaya)

Changamoto kubwa niliokutana nayo so far ni mvua kuondoka MAPEMA haswa kwenye eka nilizo lima mwishoni, vinginevyo ningepata hata wastani wa gunia 5-7 kwa eka

Next season nitarudi nikiwa na nguvu zaidi na ari zaidi
Ukwaju
 
Mwanzo mzuri next time utapat zaidi
 

Hongera mkuu nilivutiwa na uzi wako nimekua mfatiliaji umenifundisha kitu. Hope nami siku ntaingia shamba. Ntalima zao la kibiashara na zao la chakula. Hujasema gharama za kutunza au wewe ulikua na stoo teyari

Tukutane kwa muhindi. Kongore [emoji122]
 

Mkuu sehemu ya kuhifadhi ipo free kabisa
Huku ni kwetu kabisa kijijini ipo nyumba ya dingi ina nafasi ya kutosha kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…