Naiona hatari huko mbele uteuzi wa wanajeshi walio kazini kushika nyadhifa za kisiasa

Naiona hatari huko mbele uteuzi wa wanajeshi walio kazini kushika nyadhifa za kisiasa

Japo sina muda wa kutoa orodha ya teuzi kama hizi na athari zake kwa historia ya dunia.

1. Katiba inakataza majeshi yetu kujihusisha na siasa kwa maana nyingine majeshi wao huwa pale kulinda katiba na sheria hawatakiwi kuwa na chama, na kwa ufupi wanatakiwa kutii kwanza katiba then wanakuja kwenye sheria , then rais kama amiri jeshi mkuu.

2. Ila bahati mbaya kwetu imegeuzwa anatangulia rais then sheria na ya mwisho katiba.

3. Liko wazi awamu ya tano kama wewe huna kadi ya CCM huwezi kuteuliwa nyadhifa yoyoyte ya kisiasa inayoambatana na uteuzi.

4. Toka enzi ya mwalimu wakuu wa mikoa hasa wa mipakani aliteuwa wastaafu kushika nyadhifa hizo alijua kuwa walishaondoka jeshini na nafsi zao zinawatu wengine.

Cha ajabu awamu hii inawatoa askati jeshini inawapa nafasi za kisiasa hii ni hatari sana kuchanganya jeshi na utawala wa kiraia hasa kwa baadae hii tabia ikiendelea.

5. Hawa wanajeshi wakizoea hili na ili wajihakikishie kupata uteuzi na wao kwa kiasi kikubwa ndio wamepewa mamlaka ya haki na usalama nchini watafanya yote kumfurahusha mteuzi sio kufata sheria na katiba.

Mwisho wa siku watataka wakae wao na hakuna wa kuwazuia naiyona nchi inaelekea kutawaliwa na jeshi na sio kuongozwa na raia.

View attachment 1499742
Nawasilisha kwa ufupiView attachment 1499767

Wanajeshi ni wabobezi katika mambo ya ulinzi na usalama, wamesimama katika nafasi nzuri zaidi kuongeza mkoa na wilaya kwa kuwa hawa ndiyo wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama. Mkoa iliyopo mpakani inapendeza zaidi kuongeza na wanajeshi kama wakuu wa mkoa na wilaya.Acha wivu wa kibeberu
 
Japo sina muda wa kutoa orodha ya teuzi kama hizi na athari zake kwa historia ya dunia.

1. Katiba inakataza majeshi yetu kujihusisha na siasa kwa maana nyingine majeshi wao huwa pale kulinda katiba na sheria hawatakiwi kuwa na chama, na kwa ufupi wanatakiwa kutii kwanza katiba then wanakuja kwenye sheria , then rais kama amiri jeshi mkuu.

2. Ila bahati mbaya kwetu imegeuzwa anatangulia rais then sheria na ya mwisho katiba.

3. Liko wazi awamu ya tano kama wewe huna kadi ya CCM huwezi kuteuliwa nyadhifa yoyoyte ya kisiasa inayoambatana na uteuzi.

4. Toka enzi ya mwalimu wakuu wa mikoa hasa wa mipakani aliteuwa wastaafu kushika nyadhifa hizo alijua kuwa walishaondoka jeshini na nafsi zao zinawatu wengine.

Cha ajabu awamu hii inawatoa askati jeshini inawapa nafasi za kisiasa hii ni hatari sana kuchanganya jeshi na utawala wa kiraia hasa kwa baadae hii tabia ikiendelea.

5. Hawa wanajeshi wakizoea hili na ili wajihakikishie kupata uteuzi na wao kwa kiasi kikubwa ndio wamepewa mamlaka ya haki na usalama nchini watafanya yote kumfurahusha mteuzi sio kufata sheria na katiba.

Mwisho wa siku watataka wakae wao na hakuna wa kuwazuia naiyona nchi inaelekea kutawaliwa na jeshi na sio kuongozwa na raia.

View attachment 1499742
Nawasilisha kwa ufupiView attachment 1499767
Ni sawa tu kama ilivyo kuzisoma namba ambavyo hakuchagui kada na asiye kada!!!
Gharama za kukiuka katiba zitalipwa kwa Watanganyika wote hakuna atakayepunjwa.
 
Shetani ni nani?
Umetahadharisha jambo zuri. Ni kwa faida yetu sote watanzania na nchi yetu wakiwemo CCM. Wabongo na upeo mdogo wa kuchambua mambo hawawezi kuona consequenses zake. Waache wakukebehi. Siku yakitufika matokeo yake ndiyo tutajilaumu. Hii halinishangazi sana kwani waafrika matatizo yetu mengi ni sisi wenyewe tunayatengeza.
 
Kwa taarifa fupi tu ni kwamba wakuu wa mikoa na wilaya ni sehemu ya kamati kuu ya siasa ya ccm ya mkoa/wilaya kwa hiyo hao. Askari wanaenda kufanya kazi za chama.

Katiba ya CCM iko wazi imeeleza kila kitu,usifikiri magu anawaweka bila kufikiria anajua ni wake,na ndo maana akikupa hizo nafasi mpinzani lazima utahama chama tu kwenda ccm, rejea mkuu wa mkoa kilimanjaro alihama ACT Wazarendo baada ya kuteuliwa, maana ingekuwa ngumu kufanya kwenye kamati ya siasa ya chama akiwa bado act wazarendo
Tupo kwa ajili ya kutafuta kula ya familia na maendeleo ya familia pia[emoji5]
Mkuu wa mkoa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama hivo haina shida ni sawa unamtoa samaki ziwani na kumtupa baharini
 
Kuna kitu nahisi baadhi ya wachangiaji ikiwemo G'taxi nahisi hamjakielewaa bado. Anachojaribu kuwasilisha mtoa mada ni kuwa NI HATARI SANA KWA MWANA USALAMA KUZOEA MADARAKA KAMA YA KISIASA MAANA KUNA SIKU TUSIYOIJUA ATATAMANI NA YEYE AKALIE NAFASI ILE ALIYOKALIA YULE ALIYEMTEUA KWA MAANA HAKUNA ASIYEPENDA KUABUDIWA. sasa ukifika wakati huo ndipo tutayashuhudia yale ambayo hatukuwahi kuyawaza. Mhe.Rais anaweza akahisi anakua salama zaidi akiwa na hao wanausalama kumbe labda anajiweka kwenye hatari zaidi kwa maana anawapa nafasi ya kumjua na kujua zaidi kuhusu yale wasiyoyajua.
Hivyo nadhani mtoa mada anaweza akawa mzalendo zaidi kwa hiki alichokiandika kuliko sisi wachangiaji tunaojisifia kuwa ni wazalendo na kusifia kila kitu ambacho mh. JPM anafanya. We all are appreciating to what our Beloved H.E Dr. JPM is serving for the country. But he needs to be more secured .
 
Back
Top Bottom